Na. Francisca Swai – Mahakama, Musoma
Ujumbe wa Benki ya Dunia jana tarehe 29 Machi, 2022 ulitembelea na kukagua maendeleo ya miradi ya ujenzi wa Mahakama za Wilaya Rorya na Butiama mkoani Mara zinazojengwa kwa ufadhili wa benki hiyo.
Katika
ukaguzi wa miradi hiyo inayotarajiwa kukamilika tarehe 12 Aprili, 2022, ujumbe
huo ulionesha kuridhishwa na hatua iliyofikiwa katika ujenzi na kumsisitiza
mkandarasi wa miradi hiyo ‘United Builedrs’ kuongeza kasi katika hatua
zilizobaki ili ujenzi uweze kukamilika ndani ya wakati.
Ujumbe
huo ambao waliambatana na baadhi ya watumishi wa Mahakama ya Tanzania
wakiongozwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kutoka Kitengo cha
Uboreshaji wa Huduma za Mahakama, Mhe. Sekela Mwaisege ulipata nafasi ya
kutembelea Mahakama Kuu Musoma na kusalimiana na Jaji Mfawidhi wa Mahakama, Kanda
ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya.
Akiongea
na ugeni huo, Jaji Mtulya aliwashukuru kwa kutembelea ujenzi wa Mahakama hizo mbili
za Wilaya pamoja na kuendelea kufadhili miradi ya ujenzi wa Mahakama mbalimbali
nchini, jambo linalosaidia kuboresha taswira na mtazamo kwa wananchi kuhusu huduma
za Mahakama.
Aidha,
Mhe. Mtulya alisisitiza kukamilisha miradi hiyo kwa wakati na kwa ubora
unaotakiwa. Alisema umalizaji mzuri wa
ujenzi unaozingatia ubora utasaidia kuepuka usumbufu kwa watumiaji wa majengo
hayo ya kisasa hasa katika suala zima la mifumo ya umeme na maji.
Ugeni
huo katika ukaguzi wa miradi yote miwili ya Mahakama ya Wilaya ya Rorya na
Butiama uliongozwa na Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Musoma, Bw. Festo Chonya.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (wa sita kulia)
akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Benki ya Dunia ulioongozwa na Bw.
Benjamin Mtesigwa (wa sita kushoto) pamoja na watumishi toka Makao Makuu ya
Mahakama ya Tanzania, waliongozwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania
kutoka Kitengo cha Uboreshaji wa Huduma za Mahakama, Mhe. Sekela Mwaisege
(katikati). Ugeni huo katika ukaguzi wa miradi yote miwili ya Mahakama ya
Wilaya ya Rorya na Butiama uliongozwa na Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Musoma,
Bw. Festo Chonya (wa tano kushoto).
Hongera Sana viongozi wetu kazi njema, jaji mfawidhi Mahakama kuu ya musoma nakusalimia Sana Jose huku paradise hotel
JibuFuta