Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Mhe. Dkt. John Utamwa ameongoza kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Kanda hiyo kilicholenga kuangalia mwenendo wa utekelezaji wa shughuli za Mahakama ndani ya Kanda hiyo.
Kwa mujibu wa Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Bi. Melea Mkongwa, amesema kuwa kikao hicho kilichofanyika tarehe 22 Aprili, 2022 kilijadili pia ajenda mbalimbali ikiwemo kupokea hoja za Wafanyakazi.
“Katika kikao hicho cha Baraza tulitoa taarifa ya mwenendo wa mashauri pamoja na mikakati ya uendehaji wa mlundikano wa mashauri na vilevile tumefanya uchaguzi wa Katibu na Katibu Msaidizi wa Baraza,” amesema Bi. Melea.
Kikao hicho kilichohusisha Wafanyakazi wa Mahakama kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Iringa na Njombe kilitoka na maazimio mbalimbali yakiwemo ya kuomba kuboreshewa maslahi ya Watumishi hususani mishahara na mengineyo ambayo yote yamewasilishwa kwenye Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
Matukio katika picha, kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni