Ijumaa, 29 Aprili 2022

MKUU WA SEKRETARIETI YA JMAT AJITAMBULISHA RASMI KWA MTENDAJI MKUU

 

Mkuu wa Sekretarieti ya Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT) ambaye pia ni  Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Mhe. Mary Kallomo (kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipofika ofisini kwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel leo tarehe 29 Aprili, 2022 kwa lengo la kujitambulisha rasmi kwa Mtendaji huyo.

Mkuu wa Sekretarieti ya Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT) ambaye pia ni  Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Mhe. Mary Kallomo (kushoto) akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel. Lengo la ujio wa Kiongozi huyo ofisini kwa Mtendaji Mkuu ni kujitambulisha pamoja na kuomba ushirikiano baina ya chama hicho na Mahakama ya Tanzania. Ameahidi pia Chama hicho kitashirikiana na Mahakama katika utekelezaji wa Mpango Mkakati wake (2020/2021 - 2024/ 2025).

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza jambo na Mhe. Mary (hayupo katika picha) wakati Kiongozi huyo wa JMAT alipomtembelea Prof. Ole Gabriel ofisini kwake Mahakama Rufani jijini Dar es Salaam. Prof. Ole Gabriel amemtaka kiongozi huyo pamoja na wenzake kushirikiana kutatua changamoto mbalimbali zinazokikabili chama hicho na vilevile ameahidi kutoa ushirikiano.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akimkabidhi Mhe. Mary Kallomo nakala ya Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania (2020/2021 - 2024/2025).

(Picha na Mary Gwera, Mahakama)

 

 

 

Maoni 1 :

  1. Chama Cha majaji na mahakimu kinatusaisia kuongeza bidii na ufanisi wa kazi. Naupongeza uongozi wa JMAT kwa kutuimarisha wanachama wake na uongozi wote wa Mahakama. Weledi zaidi inahitajika kwa wahe. Ili Champa kiweze kutunufaisha.

    JibuFuta