Na. Paul Paschal-Mahakama, Moshi.
Watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Moshi
wa kada mbalimbali wanaohudhuria mafunzo ya Ofisi Mtandao wamehimizwa kwenda na
mabadiliko ya kisasa yanayoendelea ndani ya Mahakama ya Tanzania.
Akifungua mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza leo
tarehe 11 April 2022, Kaimu Mtendaji wa Mahakama Kuu wa Kanda hiyo, Bw Paul Mushi
amesema Mahakama ya sasa ni ya kisasa, hivyo amewaomba watumishi hao kuhakikisha
nao wanakuwa wa kisasa kwa kujifunza kwa bidiii kadiri wanapopata fursa hizo.
“Sote ni
mashahidi, Mahakama inaboreka kwa kasi na tumshukuru Mungu tumepata watendaji
wenye spidi ya hali ya juu, hivyo ni jukumu letu pia kuunga mkono juhudi za uboreshaji
kuelekea Mahakama mtandao,” Bw. Mushi amesema
Mafunzo hayo yamejumuisha watumishi 29 wakiwemo Mahakimu,
Wasaidizi wa Kumbukumbu ,Wakaguzi wa Hesabu za Ndani, Maafisa Utumishi na Utawala
na Wahasibu kutoka Wilaya zote sita za Mkoa wa Kilimanjaro.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni