Na Magreth Kinabo – Mahakama
Jaji Mstaafu wa
Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Joaquine De Mello ameeleza
siri ya mafanikio yake kuwa imetokana na malezi ya wazazi wake waliomlea kwa
upendo na heshima, ambayo yalimfanya kushika nafasi mbalimbali za uongozi.
Ameyasema hayo leo tarehe 20 Mei, 2022 wakati akitoa
hotuba yake ya kuagwa kitaaluma yeye na mwenzake, Jaji Mstaafu Susana Mkapa kwenye
hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi namba moja wa Mahakama hiyo ulioko jijini
Dar es Salaam.
Hafla hiyo iliongozwa na Jaji Kiongozi wa Mahakama
Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani na
kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi na watumishi wa Mahakama hiyo.
Jaji De Mello ambaye amestaafu utumishi wa umma tarehe
25 Novemba, 2021 baada ya kuitumikia Mahakama hiyo kwa kipindi cha muongo mmoja.
“Mafanikio yangu yametoka kwa Baba na Mama yangu.
Nimekuwa nikifanya vizuri darasani na vile vile katika uongozi wangu tangu
utoto wangu. Aidha malezi na makuzi yangu katika dini ya Kikristiko ya
Kikatoliki ndio yameniwezesha kuwa mtu anayemwogopa na kumuheshimu Mungu,
kuwapenda na kuheshimu watu wote licha ya tofauti zetu bila kuwabagua,’’
alisema Jaji De Mello.
Aliongeza kuwa katika kipindi chake cha uongozi
amewahi kutoa maamuzi ya mashauri yenye mvuto kwa jamii, mfano shauri la mauaji
ya albino lilitotokea Geita ambako watuhumiwa walitiwa hatiani na kuhukumiwa
kunyongwa.
Aidha, Jaji huyo alisema kuwa utafiti alioufanya
aligundua kwamba muaji hayo yanatokana na imani za kichawi zilizohusishwa
katika kazi za migodini, shughuli za kisisasa za kutafuta madaraka, wadhifa na
utajiri.
Kwa upande wake, Jaji Mkapa aliyejuwa anahudumu kati Kitengo
cha Usuluhishi, alisema jukumu kuu katika utendaji kazi wa Mhimii wa Mahakama
ni utoaji haki kwa jamii, hivyo linapaswa kutekelezwa kwa uadilifu, kufanya
kazi kwa unyenyekevu, umakini, utashi, kujiamini, busara, ujasiri, uthabiti,
kutojihusisha na vitendo vya rushwa na kuzingatia utu kwenye maamuzi pasipo
upendeleo ikiwemo kuwa na hofu ya Mungu.
Naye Kaimu Jaji Mfawidhi wa Kitengo cha Usuluhishi, Mhe. Zahra Maruma alisema Jaji Mkapa ameokoa mabilioni ya fedha na muda ambao ungetumiwa na wadaawa kuendesha mashauri wakati yeye ametumia chini ya siku 30 tu kuyatatua. Aliitaja moja ya kesi ya usuluhishi nama 119 ya mwaka 2021, ambapo thamani ya fedha zilizokuwa zinadaiwa ni dola 1,311,999 iliyosuluhishwa mahakamani kwa furaha na kwenda kuendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa.
Jaji Kiongozi wa Mahakama, Mhe. Mustapher
Siyani, (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Majaji wastaafu, (wa pili
kulia) ni Jaji
Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe.
Joaquine De Mello na
(wa pili kushoto) ni Jaji Mstaafu Mkapa wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo
cha Usuluhishi, Mhe. Susana Mkapa. (Alyevaa
kilemba cha kijani) ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Barke Sahel.Wa
kwanza kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe.
Amiri Mruma na wa kwanza kulia, Kaimu Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Kitengo cha Usuluhishi, Mhe. Zahara Maruma, wengine
waliosimama ni baadhi ya Majaji na watumishi wa Mahakama.
Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kitengo cha Usuluhishi, Mhe. Zahra Maruma(kulia) akimpatia shada la maua ikiwa ni isha ya kumpongeza, Jaji Mstaafu Mkapa wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Usuluhishi, Mhe. Susana Mkapa.
Jaji Kiongozi wa Mahakama, Mhe. Mustapher Siyani, (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na wanakawaya wa Mahakama ya Tanzania waliosimama. (wa pili kulia) ni Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Joaquine De Mello na (wa pili kushoto) ni Jaji Mstaafu Mkapa wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Usuluhishi, Mhe. Susana Mkapa. Wa kwanza kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Amiri Mruma na wa kwanza kulia, Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kitengo cha Usuluhishi, Mhe. Zahara Maruma, wengine waliosimama ni baadhi ya watumishi wa Mahakama hiyo.
Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Joaquine De Mello, akiitunza kwaya ya Mahakama ya Tanzania, (haipo pichani).
Baadhi ya wanafamilia wa wastaafu hao.
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa katika hafla hiyo.
Kwaya ya Mahakama ya Tanzania ikiimba wimbo maalumu wa kuwaaga Majaji hao wanaostaafu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni