Na Evelina Odemba – Mahakama Morogoro
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya
Morogoro, Mhe. Paul Ngwembe jana tarehe 6 Mei,2022 aliwaongoza watumishi wa Mahakama
katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki mkoani hapa kwenye zoezi la upandaji miti.
Zoezi hilo lililowajumuisha viongozi na watumishi wote
na kufanikisha kupanda miti zaidi 70 katika eneo la wazi lililopo mbele ya
jengo la Kituo hicho.
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo, Mhe. Ngwembe
alisema kuwa uwepo wa matukio ya uvamizi wa maeneo ya wazi ni miongoni mwa
sababu zilizopelekea Mahakama mkoani Morogoro
kuchukua jukumu la kupanda miti hiyo ambayo licha ya kuhifadhi eneo pia lina
faida nyingi.
Alisema, “Eneo hili la wazi ni kubwa ambalo linaweza kuja kutumika baadae
kwa shuguli za Mahakama, hivyo tumepanda miti jamii ya Mitiki na Mikongo
inayosifika kwa mbao na kuhifadhi ardhi vizuri”
Mhe. Ngwembe aliongeza, “Tumeona eneo hili la wazi tuliifadhi kwa
kupanda miti ambayo inafaida sana kwa kizazi hiki na kizazi kijacho cha
Mahakama.”
Akizungumza kwa niaba ya watumishi wa Kituo Jumuishi
cha Utoaji Haki, Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Morogoro, Bw. Ahmed Ng’eni
alisema kuwa upandaji wa miti ni sehemu ya maazimio yaliyowekwa kituoni hapo
ili kuhakikisha maeneo ya wazi yote yanahifadhiwa kwa namna endelevu.
“Mbali na kutupatia kivuli pia miti hii inaweza
kutumika kama chanzo cha mbao hapo mbeleni”, alisema.
Zoezi hilo lenye faida halikuweza kuathiri shuguli
za Mahakama kwani lilifanyika mara baada ya saa za kazi, ambapo Majaji,
Mahakimu, Naibu Msajili, Mtendaji na watumishi wote walifanikiwa kupanda miti,
huku Mhe. Ngwembe akimtaka kila mmoja kuutunza mti alioupanda ndani ya miezi
sita.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro, Mhe. Paul Ngwembe akipanda
mti katika eneo la wazi kwenye Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Morogoro.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro, Mhe. Messe Chaba akishiriki zoezi la upandaji miti.
Mtendaji
wa mahakama kuu kanda ya Morogoro Ahmed Ng'eni akishiriki zoezi la upandaji
miti.
Naibu
Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya
Morogoro, Mhe. Sylivester Kanda akipanda
miti.
1. Maafisa
kumbukumbu kutoka Mahakama Kuu, Boniphase Masubo (kulia) Respisious Kaijage (katikati)
na Blanka Muhume (kushoto) wakishiriki zoezi la upandaji miti.
1. Hakimu
Mkazi wa Mahakama ya Mkoa Morogoro, Mhe. Manyama akipanda mti.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni