Na Tiganya Vincent, Mahakama ya Tanzania
Jaji
Mkuu wa Uganda, Mhe. Alfonse Chigamoy Owinyi- Dollo amesema wametembelea Chuo
cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kwa ajili ya kubadilishana uzoefu wa
jinsi ya kuwandaa maafisa wa Mahakama ambao wamepangiwa majukumu mapya.
Alisema
wanataka kupata uzoefu ambao utawasaidia yeye na ujumbe kutoka Chuo cha
Mahakama cha Uganda kuwawezesha watumishi wanaopewa majukumu mapya kupata
mafunzo ambayo yatasaidia katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Mhe.
Owinyi- Dollo ametoa kauli hiyo leo tarehe 25 Mei, 2022 mjini Lushoto wakati
ziara yake na Watumishi wa Chuo cha Mahakama cha Uganda ya kutembelea na kubadilisha
uzoefu na Chuo cha Uongozi wa Mahakama cha Lushoto.
Alisema
mafunzo ya kuwandaa maafisa wa Mahakama waliopewa majukumu mapya ni muhimu
katika kuhakikisha kuwa kunakuwepo huduma bora ya utaoji haki kwa wananchi.
“Maafisa
wa Mahakama walioandaliwa kwa kupewa mafunzo mazuri wataelewa vema majukumu yao
na mambo ambayo anatakiwa kufanya katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma
za kupata haki wanapokuwa na mashauri” alisema
Katika
hatua nyingine, Jaji Mkuu wa Uganda amesema kupitia Serikali wako katika
uboreshaji wa utoaji wa huduma ya haki kwa wananchi kwa ajili ya kupeleka
maeneo yaliyo mbali.
Alisema
hatua hiyo inalenga kuwawezesha wananchi wasiokuwa na uwezo wa kupata fedha za
kusafiri umbali mrefu na kupeleka Mashahidi wakati wa kutafua haki zao.
Mhe.
Owinyi-Dollo alisema maafisa wanaopewa majukumu katika mahakamani vema
wakaandaliwa ili waweze kujua majukumu yao kabla ya kuingia katika Vituo vyao
vipya vya kazi kwa ajili ya kuwafanya wahakikishe wanatoa huduma za kiwango bora
kwa wananchi.
Kwa
upande wa Mkuu wa Chuo wa Mahakama cha Uganda, Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe.
Damalie Lwanga amesema wao bado hawajaanza kutoa kozi Astashahada na Statashaha
ya Sheria bali wanatoa kozi ambazo kwa ajili ya kuwasaidia maafisa wa Mahakama
ambao wako kazi na wanaotarajia kustaafu.
Ameyataja
mafunzo ambayo wanatoa ni pamoja na maafisa wa Mahakama wakiwemo Majaji na
Mahakimu kukabiliana na msongo wa mawazo(stress) zinazotokana na majukumu,
masuala ya afya na maandalizi ya
kustaafu.
Naye
Jaji wa Mahakama ya Rufaa ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi cha Lushoto, Mhe.
Dkt. Paul Kihwelo amesema kuwa wanachuo wanaohitimu na kujiunga na Vyuo vikuu
hapa nchini wamekuwa wakifanya vizuri kitaaluma.
Sehemu ya Mahakimu kutoka Mahakama ya Wilaya ya Lushoto wakifuatilia hotuba hizo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni