Na Francisca Swai-Mahakama, Musoma.
Mahakama
Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma imetekeleza kwa vitendo agizo alilolitoa Jaji Mkuu
wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma kwenye ziara yake mwaka jana ya
kutunza mazingira yanayozunguka maeneno mbalimbali ya Mahakama, hususani katika
jengola kisasa la Mahakama Kuu.
Hayo
yalijidhihirisha jana tarehe 14 Juni, 2022 kufuatia jopo la Majaji wa Mahakama
ya Rufani linaloongozwa na Mhe. Dkt Gerald Ndika kutembelea maeneo ya Mahakama
Kuu Musoma na kujionea uzuri wa mandhari ya eneo hilo. Majaji wengine ni Mhe.
Winfrida Korosso na Mhe. Omar Makungu.
Majaji
hao ambao wapo Musoma mjini mkoani Mara kwenye kikao cha Mahakama ya Rufani kinachofanyika
katika jengo la Mahakama Kuu wameonyesha kufurahishwa na jitihada zinazofanywa
na Kanda hiyo katika kutunza mazingira.
Ili
kuunga mkono juhudi hizo, Majaji hao walishiriki katika zoezi la kupanda miti
katika eneo hilo la Mahakama Kuu Musoma. Kikao hicho cha Mahakama ya Rufani kilichoanza
tarehe 30 Mei, 2022 kinatarajiwa kukamilika tarehe 17 Juni, 2022.
Jopo
la Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani walioko Mahakama Kuu Musoma kwa
ajili ya kikao cha Mahakama ya Rufani kilichoanza tarehe 30 Mei, 2022 na
kinatarajiwa kukamilika 17 Juni, 2022, wameonesha kuridhishwa na utunzaji wa
mazingira walipokuwa katika zoezi la upandaji miti leo 14 Juni, 2022 katika
Mahakama hiyo.
Muonekano wa eneo la mbele wa jengo la Mahakama Kuu Musoma.
Mwenyekiti wa Jopo la Majaji watatu wanaoendelea na usikilizwaji wa mashauri Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Dkt. Gerald Ndika akipanda mti katika eneo la bustani la Mahakama Kuu Musoma.
Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Winifrida Beatrice Korosso akipanda mti katika eneo la bustani la Mahakama Kuu Musoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni