Na Tiganya Vincent-Mahakama –Dodoma
Majaji
wapya wametakiwa kusoma kila mara na kuielewa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025
ili waweze kutambua mwelekeo wa nchi na maeneo ambayo yanawahusu wakati wa
utekelezaji wa majukumu yao.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma wakati
akifungua mafunzo elekezi kwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania ambao
wameapishwa jana na Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Amesema
katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 inaelezea kuhusu kujenga mazingira ya
amani, usalama na umoja Tanzania ambao Majaji wanamchango mkubwa katika
kutekeleza lengo hilo.
Mhe.
Prof. Juma amesema kuwa Jaji mahiri ni yule atakayeelewa kuwa majukumu yake ya
utoaji haki yana mchango mkubwa kwa Tanzania katika kuwepo wa mazingira ya amani
, usalama na umoja nchini.
Ameongeza
kuwa eneo jingine ni lile ambalo linaelezea kujenga utawala wa sheria, utawala
bora ambapo Majaji wanamchango mkubwa katika eneo hilo.
Wakati
huo huo, Jaji Mkuu amewataka Majaji wapya kuishi kwa kuzingatia uzito wa viapo
vyao, ahadi ya uadilifu na Kanuni za Maadili za Maafisa wa Mahakama ili wawe
salama katika utekelezaji wa majukumu yao.
Amesema
sanjari na hilo amewataka kutoonyesha hisia zao wazi wazi kwa kuwa kunaweza
kupewa tafsiri ya upendeleo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha
Mhe. Prof. Juma ametahadhari Majaji wapya kutoshiriki na kutoa maoni kupitia
mitandao ya kijamii kama vile whatsapp,
Facebook, instagram, twitter.
Mhe.
Prof Juma ametaka kutathmini na kupanga upya orodha ya marafiki, aina za
biashara, maeneo ya starehe, washirika wa kibiashara.
Amesema
lengo kuwataka wajilinde kujilinda na mitazamo ambayo mwananchi wa kawaida
anaweza kuwa nayo akiona Jaji akijumuika na mwananchi aliye na shauri mbele
yake.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akifungua leo mafunzo elekezi kwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu ya Zanzibar leo tarehe 30 Agosti, 2022 katika Ukumbi wa mikutano wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Dodoma. Kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, Mhe. Dkt. Gerald Ndika na kulia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe Mustapher Siyani
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe Mustapher Siyani akitoa neno la shukrani mara baada ya ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu ya Zanzibar leo tarehe 30 Agosti, 2022 katika Ukumbi wa mikutano wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Dodoma. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma.
Sehemu ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu ya Zanzibar wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (hayupo pichani)
Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, Mhe. Dkt. Gerald Ndika akitoa neno kwa Majaji (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu ya Zanzibar, wa tatu kulia ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, wa pili kulia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani na wa kwanza kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson Mdemu.
Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, Mhe. Dkt. Faustine Kihwelo akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu ya Zanzibar, Kulia ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma na katika ni Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, Mhe. Dkt. Gerald Ndika.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu ya Zanzibar mara baada ya kufungua mafunzo elekezi kwa Majaji hao. Wengine ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe Mustapher Siyani (wa tatu kulia),Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, Mhe. Dkt. Gerald Ndika (wa tatu kushoto), Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, Mhe. Dkt. Faustine Kihwelo (wa pili kushoto), Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson Mdemu (wa pili kulia), Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (wa kwanza kushoto) na Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Wakili Genoveva Katto.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Majaji Wanawake wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu ya Zanzibar mara baada ya kufungua mafunzo elekezi kwa Majaji hao. Wengine ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe Mustapher Siyani (wa tatu kulia),Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, Mhe. Dkt. Gerald Ndika (wa tatu kushoto), Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, Mhe. Dkt. Faustine Kihwelo (wa pili kushoto), Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson Mdemu (wa pili kulia), Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (wa kwanza kushoto) na Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Wakili Genoveva Katto.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama mara baada ya kufungua mafunzo elekezi kwa Majaji hao. Wengine ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe Mustapher Siyani (wa tatu kulia),Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, Mhe. Dkt. Gerald Ndika (wa tatu kushoto), Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, Mhe. Dkt. Faustine Kihwelo (wa pili kushoto), Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson Mdemu (wa pili kulia), Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (wa kwanza kushoto) na Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Wakili Genoveva Katto.
Sehemu ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu ya Zanzibar wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (hayupo pichani)
Sehemu ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu ya Zanzibar wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (hayupo pichani)
(Picha na Innocent Kansha - Mahakama, Dodoma)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni