Na Castilia Mwanossa-SAUT
Katibu wa Jaji Mkuu
Zanzibar, Hakimu Mkazi, Mhe. Mohammed Suleiman Omar leo tarehe 31 Agosti, 2022 amemtembelea
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel na kufanya
naye mazungumzo mafupi.
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Omar alitoa shukurani kwa niaba ya wenzake watatu Sarah Hafidh, Zired Msanif na Asya Ali kwa mafunzo elekezi waliyoyapata hivi karibuni. Kadhalika, Katibu huyo wa Jaji Mkuu wa Zanzibar alikabidhi ripoti ya mafunzo hayo.
Amezungumzia jinsi
walivyopata mafunzo ya kubadilishana uzoefu wa kusimamia na uendeshaji wa kesi
mahakamani kwa muda wa miezi miwili na
kufurahishwa jinsi Kituo Jumuishi cha Kinondoni kinavyofanya kazi.
Hakimu Mkazi na Katibu wa Jaji Mkuu Zanzibar, Mhe. Mohammed Suleiman Omar (kushoto) akimkabidhi Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia ripoti ya Mafunzo hayo.
(Picha na Margreth Kinabo-Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni