·Wapo watumishi nane wa Mahakama ya Tanzania
Na
Faustine Kapama-Mahakama, Morogoro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia
Suluhu Hassan ameteua maafisa 22 kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi ya Mawasiliano ya
Rais Ikulu, Bi Zuhura Yunus usiku wa kuamkia leo Agosti 6, 2022 imesema uteuzi
huo umefanyika Agosti 4, 2022 na wateule hao wataapishwa tarehe itakayotangazwa
baadaye.
Walioteuliwa ni Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Kevin
Mhina, Wakili Mkuu wa Serikali, Bw. Gabriel Malata, Naibu Msajili wa Mahakama na
Katibu wa Jaji Mkuu, Mhe. Adrian Kilimi na Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama
ya Rufani, Mhe. Happiness Ndesamburo.
Taarifa hiyo imewataja maafisa wengine akiwemo Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Victoria
Nongwa, Naibu Msajili na Katibu wa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania,
Mhe. Obadia Bwegoge na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Mhe. Ruth Massam.
Wengine ni Naibu Msajili na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi
wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mhe Godfrey Isaya, Naibu Msajili wa
Mahakama Kuu, Mhe. Gladys Barthy na Mwendesha Mashitaka Mfawidhi Mahakama Kuu,
Zanzibar, Bw. Haji Suleiman Haji.
Uteuzi huo unawajumuisha pia Kamishna Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora, Bi Fatma Khalfan, Wakili wa Serikali, Bw. Abubakar Mrisha
na Wakili Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Lusungu Hongoli.
Wengine ni Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
wa Serikali, Bi Monica Otaru, Mkurugenzi Msaidizi (TAMISEMI), Bw. Kamana Kamana,
Mkurugenzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Hamidu Mwanga na Mkurugenzi wa
Sheria, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin Komba.
Uteuzi huo unawajumuisha pia Mhadhiri Msaidizi, Chuo
Kikuu Mzumbe, Dkt. Mwajuma Juma, Mhadhiri, Chuo Kikuu Dar es Salaam, Dkt.
Cleophas Morris, Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mjumbe wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC), Asina Omari, Wakili wa Kujitegemea, Bi. Aisha Bade na Wakili
mwingine wa Kujitegemea, Bw. Mussa Pomo.
Mhe. Adrian Kilimi.
Mhe. Happiness Ndesamburo.
Mhe. Victoria Nongwa.







Hakuna maoni:
Chapisha Maoni