Jumapili, 7 Agosti 2022

TANZIA; MLINZI MAHAKAMA YA MWANZO MAKERE KASULU AFARIKI DUNIA

 TANZIA

Bw. Zabron Yakobo Ndabichunde enzi za uhai wake.

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake aliyekuwa Mlinzi Mwandamizi wa Mahakama ya Mwanzo Makere Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Bw. Zabron Yakobo Ndabichunde.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma, Bw. Ndabichunde alifikwa na umauti mnamo tarehe 05 Agosti 2022 majira ya saa 10 jioni kwa ajali ya pikipiki iliyotokea eneo la Nyamidaho Makere.

Taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu Makere ambapo anatarajiwa kupumzishwa leo tarehe 07 Agosti, 2022. 

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni