Jumanne, 9 Agosti 2022

WENZA WA MAJAJI WAFANYA MATEMBEZI KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA NANENANE

 

Wanachama wa chama cha Wenza wa Majaji wanaojulikana kwa jina la “We are Family” wakiwa kwenye Matembezi Maalum yaliyolenga kusherehekea sikukuu ya wakulima (Nanenane) jana jijini Dar es salaam. Matembezi hayo yalifanyika kuanzia saa 12:30 asubuhi yakianzia nyumbani kwa Jaji Mkuu Oysterbay na kumalizikia Serena Hotel. Wa pili kushoto (katikati) ni Mwenza wa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mama Marina Juma ambaye ndiye mlezi wa chama hicho kilichoanzishwa kwa lengo la kusaidiana katika raha na shida.  Wa kwanza kushoto ni Mwenza wa Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman, mama Saada Chande ambaye aliwakilisha wenza wa Majaji Wastaafu kwenye Matembezi hayo. Chama hicho mpaka sasa kina wanachama 36 jijini Dar es salaamn na kwenye kanda mbalimbali za Mahakama Kuu.    Mwenza wa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mama Marina Juma (kushoto) akiwa na Mwenza wa Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman, Mama Saada Chande ambaye aliwakilisha wenza wa Majaji Wastaafu kwenye Matembezi  yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam. Baadhi ya Wenza wa Majaji wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa Matembezi hayo yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam. Mwenye fulana nyeupe ni Mwenza wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mama Suzan Feleshi. Kulia ni Beatrice Mdemu akifuatiwa na Yusta Mugeta, Fauzia Ismail, na Akandokola Galeba. Kutoka kushoto ni Stella Kakolaki, akifuatiwa na Doris Wambali.  

Baadhi ya Wenza wa Majaji wakiwa kwenye Matembezi hayo yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam. Wa kwanza kulia ni mama Devotha Ndika na kushoto ni mama  Zawadi Luvanda. Wenza wa Majaji wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza Matembezi katika Hotel ya Serena jijini Dar es salaam. Wa kwanza Kushoto (waliokaa) ni mama Anzanukye Ngwembe na wa kwanza kulia (waliosimama) ni mama Beatrice Mwenempazi.Wenza wa Majaji wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza Matembezi jana jijini Dar es salaam.Wenza wa Majaji wakipata kifungua kinywa mara baada ya kumaliza Matembezi ambapo pia walifanya kikao kifupi.Wenza wa Majaji wakiwa katika picha ya pamoja Serena Hotel mara baada ya kumaliza Matembezi.Mlezi wa Chama cha Wenza wa Majaji Mama Marina Juma (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenza wa Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman, Mama Saada Chande ambaye aliwakilisha wake wa Majaji Wastaafu kwenye Matembezi hayo.Mlezi wa Chama cha Wenza wa Majaji Mama Marina Juma (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenza wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dkt. Eliezer Feleshi, mama Suzan Feleshi mara baada ya kumalizika kwa Matembezi hayo.

Picha na Lydia Churi-Mahakama





















Hakuna maoni:

Chapisha Maoni