Na
Magreth Kinabo – Mahakama
Bodi ya Udhamini wa Taarifa
za Majuzuu ya Sheria Tanzania,imeanza kikao chake cha kujadili majuzuu ya mwaka
2021 na 2022 chini ya uwenyekiti wa bodi hiyo Mhe. Jacob Mwambegele, ambaye pia ni Jaji wa
Mahakama ya Rufani Tanzania.
Kwa mujibu
wa Mratibu wa bodi hiyo, Mhe. Kifungu Mrisho, alisema kikao hicho kilichoaanza
leo tarehe 12 Septemba, 2022 kitafanyika kwa muda wa siku tatu katika ukumbi wa
maktaba uliopo katika Mahakama ya Rufani Tanzania, alisema Bodi hiyo iliyochini
ya Jaji Mkuu inatoa Juzuu la Taarifa za Sheria kila mwaka.
“Leo tumeanza kikao cha
kujadili kuandaa za Taarifa za Mazuu ya Sheria ya kila mwaka,” alisema Mhe.
Kifungu.
Alisema bodi imeanza
kikao chake cha kuchambua maamuzi ya Mahakama ya Rufani, Mahakama Kuu ya
Tanzania Bara na Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa kitabu cha mwaka 2021 na pia
imejipanga kukamilisha kitabu cha mwaka 2021 na 2022.
Mhe. Mrisho aliongeza
kwamba baada ya kukamilicha kitabu cha mwaka 2021na 2022 kitaanza kuchambua
kitabu cha kila mwaka kwa kuanzia mwaka 2023.
Mwenyekiti wa kikao cha Bodi ya Udhamini wa Taarifa za Majuzuu la Sheria Tanzania, Mhe. Jacob Mwambegele , ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania akiendesha kikao hicho kilichoaanza leo tarehe 12 Septemba, 2022 na kinarajia kufanyika kwa muda wa siku tatu kwenye ukumbi wa maktaba wa Mahakama ya Rufani Tanzania uliopo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuandaa Juzuu la mwaka 2021 na 2022.
Katibu wa bodi hiyo
Prof. Ismail Majamba (wa kwanza kulia) akijadili jambo katika kikao
hicho.
Wajumbe wa kikao hicho wakiwa
katika kikao cha kuaandaa Majuzuu hayo.
Wajumbe wa kikao hicho wakiwa
katika kikao cha kuaandaa majuzuu hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni