Katika
kuhakikisha Majaji wapya wanafikia viwango vinavyokubalika katika shughuli zao
za kila siku, wameendelea kupokea mafunzo elekezi yatakayowasaidia kumudu
majukumu hayo. Sehemu ya mada hizo zilizotolewa na Wakufunzi mbalimbali ni pamoja
na Viashiria vya Rushwa kwenye Muhimili wa Mahakama kwa kuzingatia hali ya
rushwa nchini, Kanuni za maadili ya mtumishi na Uongozi wa Umma kwa Waheshimiwa
Majaji, Kanuni ya utenganisho wa mamlaka kati ya Mihimili mitatu ya Dola “Doctrine
of Separation of Powers”.
Maeno
mengine ni Jukumu la upelele wa makosa ya jinai katika usimamizi wa haki Tanzania,
Mambo yanayohusu utawala wa kimahakama, Tume ya Maadili ya Majaji na kazi zake
za msingi, Itifaki, Adabu njema na uzalendo na mada ya Ustawi wa maisha ya kila siku kwa kujali usawa.
Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mhe. Augustine Mwarija (aliyesimama mbele kulia) akitoa mada ya Tume ya Maadili ya Majaji na majukumu yake ya kila siku kwa Waheshimiwa Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakati wa mafunzo hayo elekezi.
Mtendaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Bw. Solanus Nyimbi akitoa mada ya Kanuni ya utenganisho wa mamlaka kati ya Mihimili mitatu ya Dola “Doctrine of Separation of Powers” na mambo yanayohusu utawala wa kimahakama kwa Waheshimiwa Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakati wa mafunzo hayo elekezi.
Mtaalamu wa masuala ya Ushauri, Saikolojia na mitindo ya maisha, Bi. Sadaka Gandi akitoa elimu kwa Waheshimiwa Majaji namna bora ya
Mtaalumu Kutoka Jeshi la Polisi Makao Makuu SACP Gemini Mushy (aliyesimama mbele) akitoa mada ya Jukumu la Upelelezi wa makosa ya jinai katika usimamizi wa haki jinai nchini Tanzania.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Victoria Nongwa akichangia mada wakati wa Mafunzo elekezi kwa Majaji hao
Mmoja wa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania akichangia mada wakati wa mafunzo elekezi kwa Majaji hao, (kulia aliyesimama) ni Mwezeshaji wa Mafunzo hayo Bi. Sadaka Gandi.
(Picha na Innocent Kansha - Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni