Maeneo waliyopitishwa na wakufunzi ni kama yafuatayo, Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania wa mwaka 2020/2021 hadi 2024/2025 na utekelezaji wake. Utekeleaji wa Mradi wa maboresho katika utendaji wa shughuli za Mahakama ya Tanzania za kila siku.
Hata
hivyo, maeneo mengine ni Matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
katika kufikia safari ya Mahakama Mtandao. Upandishwaji wa maamuzi ya Mahakama
katika Mfumo wa Kielektronik wa Mahakama ya Tanzania ujulikanao kama “Tanzania
Legal Information Institute” TANZLII.
Sehemu ya Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa wanamsikiliza Mkurugenzi wa Mipango na Ufuatiliaji wa Mahakama ya Tanzania Bw. Erasmus Uisso mtoa mada ya namna bora ya kutekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama (hayupo picha)
Mkuu wa Kitengo cha Uboreshaji wa Huduma za Mahakama ya Tanzania, Mhe. Dkt. Angelo Rumisha akitoa mada kwa Majaji ya namna bora ya Utekeleaji wa Mradi wa maboresho katika utendaji wa shughuli za Mahakama ya Tanzania za kila siku na mafanikio ya Mradi wa Mpango Mkakati wa Mahakama awamu ya kwanza.
Sehemu ya Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa wanamsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Uboreshaji wa Huduma za Mahakama ya Tanzania, Mhe. Dkt. Angelo Rumisha akielezea mafanikio ya Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania awamu ya kwanza (hayupo picha)
(Picha na Innocent Kansha - Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni