Na Magreth Kinabo – Mahakama
Mtendaji Mkuu wa
Mahakama ya Tanzania, Prof.Elisante Ole Gabriel leo tarehe 5 Septemba, 2022 amemkabidhi
Mkuu wa Kitengo Usimamizi wa Ujenzi(HEM),
Mhandisi Yohana Mashausi gari maalum kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa
mahakama mbalimbali nchini.
Makabidhiano hayo
yalifanyika kwenye eneo la viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini
Dar es Salaam, ambapo Mtendaji huyo alisema gari hilo aina ya Isuzu TATA lenye
namba ya usajili STM 1562 litasaidia kurahisisha ukarabati na ujenzi wa
mahakama mbalimbali nchini.
“Nimekukabidhi gari
hili ili liweze kusaidia kurahisisha shughuli za ukarabati na ujenzi wa
mahakama,”alisema Prof. Gabriel.
Kwa upande wake
Mhandisi Mashausi, alisema anashukuru kwa kukabidhiwa gari hilo, ambalo
litakuwa kitendea kazi chenye msaada mkubwa kwenye ujenzi wa Mahakama za Wilaya
na Mahakama za Mwanzo kwa kuwa mahitaji ni mengi.
Hii ni mara ya pili kwa
Mtendaji huyo kukabidhi gari kwa ajili ya shughuli za usafirishaji. Mara ya
kwanza alikabidhi mabasi mawili ambayo ni maalum kwa usafiri wa watumishi.
Mtendaji Mkuu wa
Mahakama ya Tanzania, Prof.Elisante Ole Gabriel leo tarehe 5 Septemba, 2022
akikagua gari kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa mahakama mbalimbali nchini
kwenye eneo la viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es
Salaam. Mtendaji Mkuu wa
Mahakama ya Tanzania, Prof.Elisante Ole Gabriel leo tarehe 5 Septemba, 2022 akiendesha
gari kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa mahakama mbalimbali nchini kwenye eneo la
viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Ununuzi
na Ugavi wa Mahakama Tanzania, Bw.
Charles Challe (wa pili kulia) akimkabidhi
funguo za gari Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole
Gabriel (wapili kushoto)kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa mahakama mbalimbali
nchini leo tarehe 5 Septemba ,2022 kwenye
eneo la viwanja vya Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa
Mahakama ya Tanzania, Prof.Elisante Ole Gabriel (wa pili kushoto) leo tarehe 5 Septemba 2022 akimsikiliza jambo kutoka kwa Mkurugenzi wa
Ununuzi na Ugavi wa Mahakama ya
Tanzania, Bw. Charles Challe ( wa pili
kulia) mara baada ya kukabidhiwa funguo
za gari kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa mahakama mbalimbali nchini kwenye
eneo la viwanja vya Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam.(Wa kwanza kushoto) ni Mtendaji wa Mahakama
Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha na (wa kwanza kulia) ni ni Mkuu wa Kitengo
cha Usimamizi wa Ujenzi cha Mahakama ya Tanzania (HEM) Mhandisi Yohana
Mashausi. Mkuu wa Kitengo cha
Usimamizi wa Ujenzi cha Mahakama ya Tanzania, Mhandisi Yohana Mashausi (wa pili
kushoto) akizungumza jambo mara baada ya
kupokea gari kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa mahakama mbalimbali nchini kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania,
Prof.Elisante Ole Gabriel leo tarehe 5 Septemba,2022 kwenye eneo la viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni