Na Castilia Mwanossa
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel ameipongeza Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kwa kutimiza miaka 10 na ameishauri kutatua changamoto wanazoambiwa kuhusu huduma hiyo.
Prof Gabriel alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari tarehe 5, Septemba 2022, ofisi kwake Jijini Dar es Salaam na kumshauri Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Kituba kuendelea kuangalia mamlaka hiyo kwa jicho la pekee kwakuwa ndiyo inayobeba umma kwa ujumla kwenye masuala ya mtandao.
“Ninawaomba muendelee kutoa elimu kwa umma na kuhakikisha watendaji wakuu wote wanafikiwa na kuelimishwa ipasavyo ili ifike hatua barua kutoka wizara moja kwenda wizara nyingine inatumwa kwa njia ya Serikali Mtandao kwa kuwa hatua hiyo itasaidia kupunguza mlundikano wa makaratasi katika wizara husika,” alisema Prof.Gabriel.
Aidha ameongeza kwamba elimu hiyo inatakiwa kutolewa kwa wananchi wa ngazi ya chini na watoto waliopo mashuleni ili wakue wakijua kuna Serikali Mtandao kwa sababu ni njia itakayo wasaidia kizazi kijacho kuzoea kupata huduma za kidijitali. Pia huduma hiyo italeta tija na manufaa ya kiuchumi na siyo kuharibu maisha ya kawaida.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni