·Namna ya kukabiliana na makosa yanayofanywa Majini na Baharini
Na
Innocent Kansha - Mahakama
Ofisi
ya Umoja wa Mataifa inayopambana na madawa ya kulevya, uhalifu na makosa ya
jinai “United Nations on Drugs and Crime” (UNODC) kwa kupitia mradi wa
kupambana na makosa yanayofanywa Majini na Baharini Duniani “Global Maritime
Crime Programme” (GMCP), leo tarehe 12 Septemba, 2022 imeanza kuendesha mafunzo
kwa wadau wa utoaji haki jinai kwa njia ya Mahakama ya mfano “Simulated Trial”.
Mafunzo
hayo ya Mahakama ya Mfano yanafanyika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni
(IJC) jijini Dar es salaam kwa kipindi cha siku tano kuanzia tarehe 12 hadi 16
Septemba, 2022 yanalenga kuwajengea uwezo wadau wa utoaji haki jinai kwa namna ya
kupambana na makosa yanayotendwa baharini kama vile uharamia, biashara ya usafirishaji
haramu wa binadamu, biashara haramu ya binadamu na biashara ya bidhaa haramu.
Katalogi
hiyo ya mafunzo itasaidia kuimarisha mfumo wa uendeshaji mashauri ya aina hiyo
kwa upande wa Muhimili wa Mahakama, Waendesha mashtaka na Mawakili namna bora
ya uendeshaji wa mashauri na makosa ya aina hiyo
Maeneo
mengine yatakayofaidika na programu hiyo ya Mahakama ya mfano ni uchunguzi,
uandaaji na uendeshaji wa mashauri na mwenendo wa mashauri mahakamani kwa
kupitia makosa yanayofanywa majini na baharini
Mazoezi
haya yanalenga kubainisha chagamoto za kiutendaji ikiwemo uandaaji wa mashauri,
namna ya upokeaji wa ushahidi mahakamani, namna Mawakili wavyowawakilisha
wateja wao mahakamani na mamna ya kuivutia Mahakama itoe ushindi kwa upande
mmoja wapo.
Lengo kuu la kufanya
Mahakama ya mfano ni kumaliza kisheria tatizo la makosa yanayotendwa majini na
baharini kwa kuimarisha mifumo ya mamlaka ya kijinai na kiutendaji katika nchi
mbalimbali ili kusikiliza, kuamua na kuendesha mashauri yanayohusiana na makosa
ya uharamia, usafirishaji wa madawa ya kulevya na makosa mengineyo kwa ufanisi.
Kwa
kushirikiana na wadau wa kimataifa UNODC GMCP itaendelea kuwajengea uwezo
maafisa na vyombo ya usimamizi wa sheria za bahari ili waweze kukusanya
ushahidi na kutunza wakati wa operesheni ili ushahidi huo uweze kutumiwa na
waendesha mashtaka na maafisa wa Mahakama.
Ushirikiano wa
taasisi hizi za utoaji haki jinai zitafikia hatua ya kuendesha mashauri ya makosa
hayo kwa weledi na kutoa maamuzi ya haki kwa kudhibiti na kusimamia ipasavyo makosa
yote ya aina hiyo. Hatimaye itasaidia kukabidhi na kuwasilisha ushahidi kwa
ajili ya kuendesha mashauri na kufikia haki kwa ufanisi. Malengo yake ikiwa ni
kuhakikisha makosa haya hayajirudii na hili litafanyika kupitia mafunzo hayo ya
kesi ya mfano.
Ili kupata matokeo chanya
kupitia mafunzo hayo UNODC GMCP wanashirikiana INTERPOL kutoa elimu ya Mahakama
ya mfano na baadhi ya nchi katika ukanda wa bahari ya Hindi na ukanda wa
Magharibi yamekwisha fanyika ikiwa ni pamoja na Kenya, Uganda, Seychelles na
Mauritius.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni