Na Evelina Odemba – Mahakama Morogoro
Mahakama mkoani Morogoro imekubaliana na wadau wake kuanza
kusikiliza kesi kuanzia asubuhi ili kuharakisha huduma za utoaji haki kwa wananchi.
Hayo yameazimiwa na wadau wa Mahakama katika kikao cha
kusukuma mashauri kilichofanyika leo tarehe 28 Octoba, 2022.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro,
Mhe. Japhet Manyama, ambaye aliongoza kikao hicho alisisitiza kuwa kesi
zitaanza kusikilizwa muda uliopangwa, hivyo kila mdau asimame kwenye nafasi
yake.
Aidha, wajumbe katika kikao hicho waliazimia kuwa
walaka uliotolewa wa kuwataka mamlaka husika kuleta kesi za jinai mahakamani baada
ya upelelezi umekamika uendelee kufuatwa ili kupunguza mrundikano wa watu
magerezani.
Kikao cha kusukuma mashauri ambacho huwakutanisha
wadau wa Mahakama hufanyika kila baada ya miezi mitatu kufanya kutathmini ya
mwenendo wa mashauri na kuweka mikakati ili kuhakikisha utoaji haki unafanyika
kwa wakati na kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikijitokea.
Wadau wakifatilia kikao kwa makini.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni