Na
Magreth Kinabo – Mahakama
Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Lilian Mashaka amewataka watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia maadili mema, bidii, upendo, umoja na ushirikiano ili kuweza kutimiza jukumu la mapambano dhidi ya rushwa.
Akizungumza jana katika
hafla ya kuwaaga viongozi waliohama kwa uteuzi, watumishi waliohama na
waliostaafu wa Mahakama hiyo, iliyofanyika jana jioni, kwenye viwanja vya Divisheni hiyo, iliyoko Jijini
Dar es Salaam katika Shule ya Sheria alisema amefarijika kuona watumishi hao
wakiendelea kufanya kazi kwa kuzingatia vigezo hivyo.
“Dumisheni maadili mema
katika utendaji wa kazi sote tunatagemeana katika jukumu kubwa la mapambano dhidi
ya rushwa, Divisheni hi inangaliwa kwa jicho la pili, hivyo onesheni ukomavu wa
kazi hii.“Sijasikia mkisemwa vibaya ningesikia ningewaambia,” alisema Jaji
Lilian.
Aidha Jaji Lilian
aliwaambia kwamba maisha mazuri yanakuja kutokana kufanya kazi kwa bidii katika
mazingira magumu.
Kwa Upande wake Jaji Mfawidhi
wa Mahakama Kuu Kanda Bukoba, Mhe. Immaculata Banzi aliongeza kuwa watumishi
hao wasifanyekazi kwa kunung’unika, hivyo wafanye kazi kwa nidhamu na
kuheshimiana.
Naye Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe.
Elinaza Luvanda alisema watumishi wa divisheni hiyo kuendelea kufanya kazi kwa
kuongozwa na roho Mtakatifu katika kutenda haki kwa wananchi.Hivyo anajivunia
kuwa watumishi wenye maadili mema na kufanya kazi kwa bidii, ambapo kila mmoja
anajipanga katika kazi yake.
Akizungumza kwa niaba ya wastaafu wenzake, Bi. Mchawi Mwanasoro, ambaye alikuwa Mhudumu katika Divisheni hiyo, aliwaomba watumishi hao, kujitahidi kufanya kazi kwa moyo mmoja kswa kuwa ukifanyakazi vizuri itaonekana, ambapo pia aliwaomba kupukana na vitendo viovu.
Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Lilian Mashaka, (kulia) akipewa zawadi na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Elinaza Luvanda ikiwa ni ishara ya kuagwa baada ya kupata uteuzi, katika hafla ya kuwaaga viongozi waliohama kwa uteuzi, watumishi waliohama na waliostaafu wa Divisheni hiyo, iliyofanyika jana jioni, kwenye viwanja vya mahakamni hapo , iliyopo Jijini Dar es Salaam katika Shule ya Sheria.
Jaji wa Mfawidhi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe.
Elinaza Luvanda akimlisha keki kwa
ajili ya kumuaga Bi. Mchawi Mwanansoro, ambaye amestaafu kwa mujibu wa utumishi wa umma katika hafla hiyo.
Jaji wa Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Elinaza Luvanda akimpatia zawadi Katibu Mustasi Bi. Emmanuela Peter kwa ajili ya kumuaga baada ya kupangiwa kituo kingine cha kazi.
Watumishi waagwa wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya watumishi wakicheza Bi. Mchawi Mwanasoro,( aliyevaa kitenge) ambaye alikuwa Mhudumu katika Divisheni hiyo.
Jaji Jwa Mfawidhi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe.
Elinaza Luvanda akizungumza jambo kwenye hafla hiyo.Kushoto ni Jaji wa Divisheni hiyo, Mhe. Godfrey Issaya.
Mtendaji wa Mahakama
Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Bi. Masalu
Kisasila akitoa utambulisho katika hafla hiyo.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda Bukoba, Mhe. Immaculata Banzi (kulia) akipewa zawadi na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Elinaza Luvanda ikiwa ni ishara kuaagwa baada kupangiwa kituo kingine cha kazi.
Baadhi ya watumishi wa Divisheni hiyo wakicheza na watumishi waagwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni