Watumishi wa Mahakama za Wilaya mpya nchini zilizozinduliwa hivi karibuni wanaendelea
kupatiwa Mafunzo ya Huduma kwa mteja longo likiwa ni kuboresha utendaji kazi katika
Mahakama hizo ili wananchi waweze kupata huduma bora ya utoaji haki.
Tarehe 25 Novemba, 2022 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof.
Ibrahim Hamis Juma alizindua Mahakama ya Wilaya Busega iliyowakilisha
Mahakama nyingine mpya za Wilaya mpya 17, Mahakama hizo zilizojengwa kwa
ufadhili wa Benki ya Dunia ni pamoja na; Butiama, Rorya, Songwe, Gairo,
Mkinga, Mvomero, Kilombero, Mbogwe, Nyang'hwale, Kyerwa, Itilima, Missenyi,
Kaliua, Uvinza, Buhingwe, Kakonko na Tanganyika.
Katika siku ya tatu ya Mafunzo hayo; Mada zilizotolewa
ni pamoja na; Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania na ya Mabadiliko ya
kiutendaji (Change Management).
Yafuatayo ni matukio katika picha ya Watoa mada
mbalimbali waliotoa mada siku ya tatu (3) ya mafunzo hayo:-
Muonekano wa sehemu ya wasilisho la Mpango
Mkakati lililowasilishwa na Mkurugenzi wa Mipango na Ufuatiliaji-Mahakama ya
Tanzania, Bw. Erasmus Uisso (hayupo katika picha).
Mwezeshaji wa Mafunzo, Dkt. Andrew Msami akiendelea kuwasilisha mada, amewasisitiza watumishi kuwa chanzo cha mabadiliko kwa kuwa na mtazamo chanya (positive attitude) ili kuweza kufanya kazi zitakazoleta matokeo chanya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni