Na Lydia Churi- Tume ya Utumishi wa Mahakama-Dodoma
Wajumbe
wa kikao cha Menejimenti ya Sekretariet ya Tume ya Utumishi wa Mahakama wametembelea
na kukagua ujenzi wa jengo la Tume ya Utumishi wa Mahakama unaoendelea jijini Dodoma.
Wajumbe
hao walijionea maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo la ofisi za Tume linalojengwa kwenye
kiwanja namba 3 Block D katika eneo la NCC, pembeni ya jengo la makao makuu ya
Mahakama ya Tanzania. Ujenzi huo hivi sasa uko katika hatua ya kuweka zege
kwenye msingi kabla ya kuweka nondo (Blanding stage).
Aidha
kiwanja kinachotumika kujenga jengo hilo kina ukubwa wa mita za mraba 9,590, na
kina hati yenye namba DOM008194 iliyotolewa tarehe 22 Julai, 2022.
Kwa
mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Ugavi cha Tume ya Utumishi wa
Mahakama, Jengo hilo linatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi Bilioni 14.3 (14,300,000,000)
na Mzabuni wa jengo hilo ni CRJE (EAST AFRICA) LTD.
Mkataba
wa ujenzi ulisainiwa tarehe 7 Oktoba 2022 na Mkandarasi alikabidhiwa site tarehe
10 Oktoba, 2022. Jengo hilo linatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Juni mwaka
2023.
Tume ya Utumishi wa Mahakama imeundwa na Ibara ya 112 (1) ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha, majukumu ya
Tume yameelezwa kwenye katiba hiyo katika Ibara ya 113 (1) ikisomwa pamoja na
kifungu cha 29 cha Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 4 ya mwaka 2011. Tume
ya Utumishi wa Mahakama ni chombo cha kikatiba kilichopewa jukumu la kusimamia
uendeshaji wa Mahakama ya Tanzania.
Jengo la ofisi za Tume ya Utumishi wa Mahakama likiwa katika hatua za awali za ujenzi wake. Jengo hili linajengwa katika eneo la NCC jijini Dodoma. Ujenzi unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni, 2023.

Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha Menejimenti ya Sekretariet ya Tume ya Utumishi wa Mahakama wakiwa kwenye eneo la ujenzi jana jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha Menejimenti ya Sekretariet ya Tume ya Utumishi wa Mahakama wakiwa kwenye eneo la ujenzi jana jijini Dodoma. Mwenye miwani ni Naibu Katibu wa Tume (Nidhamu na Maadili) Bi. Alesia Mbuya.
Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha Menejimenti ya Sekretariet ya Tume ya Utumishi wa Mahakama wakiwa kwenye eneo la ujenzi jana jijini Dodoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni