TANZIA
Mahakama ya
Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake aliyekuwa Hakimu Mkazi
Daraja la I wa Mahakama ya Mwanzo Kolekero Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera,
Mhe. Tumaini John Kiyeyeu.
Kwa mujibu wa
Mtendaji wa Mahakama Kuu-Kanda ya Bukoba, Bw. Lothan Simkoko, marehemu Kiyeyeu
alifikwa na umauti yeye pamoja na mumewe tarehe 06 Desemba, 2022 kufuatia
ajali ya gari aina ya basi la kampuni ya 'Happy Nation' linalofanya safari
zake kati ya Bukoba na Dar- es -Salaam na pikipiki ambayo alikuwa amepanda na
marehemu mumewe ambapo wote wawili walifariki dunia papo hapo.
Bw. Simkoko
amesema kuwa, marehemu Tumaini ameacha watoto watatu (3) Marie miaka 15,
Junior -miaka nane (8) na Michelle mwaka mmoja (1) na miezi 7.
Mahakama
alizowahi kufanya kazi ni pamoja na; Mahakama ya Mwanzo Katoma, Mahakama ya Mwanzo
Karabagaine na mpaka umauti umemkuta alikuwa Mahakama ya Mwanzo Kolekero.
Kwa mujibu wa
Mtendaji huyo, mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa leo tarehe 08
Desemba, 2022 kwenda mkoani Mbeya kwa ajili ya mazishi.
Mahakama ya
Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza katika kipindi hiki
kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni