Jumatano, 7 Desemba 2022

TANZIA; HAKIMU MKAZI MWANDAMIZI MAHAKAMA YA MWANZO ILALA AFARIKI DUNIA

 TANZIA

Mhe. Agness Barasobian enzi za uhai wake.

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake aliyekuwa Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Mwanzo Ilala, Mhe. Agness Barasobian.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu-Dar es Salaam, Bi. Athanasia Kabuyanja, marehemu Agness alifikwa na umauti usiku wa tarehe 06 Desemba, 2022 katika Hospitali ya Agakhan alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu Goba jijini Dar es Salaam

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni