Na Magreth Kinabo – Mahakama
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel amewaomba wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kuendelea kushirikiana na Mhimili huo katika kutoa elimu juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na mauaji ili kuweza kupunguza matukio hayo.
Kauli hiyo imetolewa na
Mtendaji huyo, leo tarehe 16 Desemba, 2022 katika mkutano wake na wahariri
hao uliofanyika kwenye ukumbi wa mkutano wa Kituo wa Jumuishi cha Utoaji Haki
cha Masuala ya Familia, kilichopo Temeke Jijini Dar es Salaam baada ya baadhi ya
wahariri kuuliza Mahakama inachukua hatua gani za kupunguza vitendo hivyo.
“Mahakama inaendelea
kutoa elimu kwa wadau kupitia vipindi mbalimbali
mfano cha mubashara cha kinachojulikana kwa jina la ‘Sema na Mahakama ya Tanzania’ kinachorushwa na Televisheni
ya Taifa (TBC1) kila alhamisi saa 12:00 jioni hadi saa 1:00 usiku na Kituo cha Televisheni ya (ITV) kuanzia saa
12:00 jioni hadi saa 1:30 usiku.
‘‘Lakini elimu hiyo haipaswi
kutolewa na Mahakama pekee inatakiwa ushirikiano wa pamoja kutoka kwa viongozi wa dini, vya habari na kadhalika, hivyo tunaomba na
nyie muendelee kusaidia kutoa elimu hiyo,” alisema Mtendaji Mkuu huyo.
Katika hatua nyingine
akijibu hoja kuhusu mashauri ya ardhi yanayoendeshwa na Wazee wa Baraza la Ardhi
na gharama zake, Mkuu wa Kitengo cha
Maboresho ya Mahakama ya Tanzania, Dkt. Angelo Rumisha amesema baraza hilo haliko chini ya Mahakama.
Aliongeza kuwa baraza hilo liko chini ya Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mwenyekiti wa barza hilo anateuliwa na Waziri
husika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Bw. Deodatus Balile amesema milango iko wazi kwa Mahakama kuendelea kushirikiana na TEF kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu wananchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni