Na Innocent Kansha, Mahakama
Watumishi washauriwa kujenga tabia ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara kuepuka na kupunguza msongo wa mawazo ili kujenga afya ya akili na mwili, utamaduni huo ukizingatiwa utaimarisha utendaji kazi na kujenga misingi imara ya mahusiano kazini.
Akitoa mada katika mafunzo ya watumishi wa Mahakama za Wilaya za Rorya, Butiama, Itilima na Busenga, leo tarehe 22 Desemba, 2022 Mtaalamu wa masuala ya Usimamizi wa Msongo wa Mawazo “Stress Management” Bw. Godfrey Wawa alisema msongo wa mawazo ni mfadhaiko wa akili anaoupata mtu kutokana na taabu, tishio, kupotelewa na mtu au kitu cha dhamani kwake.
“Msongo
wa kawaida unaboresha utendaji kazi wa kila siku kwa mtumishi, msongo wa aina
hiyo unaitwa changamoto ama furusa na usimamizi wake unatokana na namna
ulivyoipokea changamoto husika”, alisema Mtaalam huyo
Changamoto
ama msongo wa kawaida ndiyo chanzo cha majibu au masuluhisho ya mambo mengi
hapa duniani. Wagunduzi wa vitu mbalimbali vinavyotumika hapa duniani walipata
changamoto na kuzitafutia ufumbuzi. Hivyo kumbe maendeleo makubwa
yaliyopatikana duniani yametokana na msongo wa kawaida ama changamoto.
Bw.
Wawa alisema, kwa upande mwingine mtumishi walio wengi hukubwa na shininikizo
la kiuchumi linasababisha msongo wa mawazo na kupelekea kufanya matendo kinyume
na maadili na miiko ya utumishi wa umma kama kudai rushwa kwa wateja wanawahudumia
na mengineyo.
Mtaalum
Wawa anasema, Changamoto zikiwa nyingi sana zinasababisha mtu/mtumishi
anashindwa kumudu majukumu yake ya kila siku. Visababishi vya changamoto
vinatokana ugumu wa shughuli za mtu anazozifanya kila siku.
Maisha
yasiyo na changamoto hayafurahishi hata kidogo. Mahusiano ya kidoa, ya kazini
na kwa jamii inayokuzunguka na mazingira kwa ujumla wake yanachangia kwa kiasi
kikubwa kusababisha changamoto ya msongo wa mawazo, alisema Mtaalum Wawa
“Athari
za msongo wa mawazo ni lukuki mtu kukosa furaha, kukosa amani, kujuta wakati
wote, kuota majinamizi, tatizo la mahusiano nyumbani na kazini. Kukosa hamu ya
chakula ama kula chakula kingi kupita kiasi, Kunenepa sana ama kukonda pia ni
matokeo msongo wa mawazo”, aliongeza mtoa mada huyo
Kupata
muda wa kutosha wa kupumzika, kufanya mchezo wa yoga, kustarehe, kulala walau
masaa sita kila siku, kupata ushauri wa mara kwa mara kutoka kwa watu wa karibu
ni njia sahihi ya kukabiliana na msongo wa mawazo, alisisitiza Bw. Wawa.
Mtaalamu wa masuala ya Usimamizi wa Msongo wa Mawazo “Stress Management” Bw. Godfrey Wawa akifafanua jambo wakati mafunzo hayo yanayendelea Mahakama Kuu, Kanda ya Musoma.
Sehemu ya watumishi wakifuatili mafunzo hayo yanayoendelea Mahakama Kuu Kanda ya Musoma.
(Picha na Innocent Kansha)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni