Jumatatu, 30 Januari 2023

BILIONI 5 ZIMETUMIKA KUKAMILISHA MAJENGO MATANO YA MAHAKAMA ZA WILAYA

Na Tiganya Vincent-Mahakama-Manyoni

Mahakama ya Tanzania imetumia zaidi ya shilingi bilioni 5 katika  kukamilisha majengo mapya ya Mahakama za Wilaya tano zilizopo kwenye mikoa ya Singida, Mara, Mbeya, Tabora na Tanga.

Akizungumza leo tarehe 30 Januari, 2023 wakati wa hafla ya uzinduzi wa Majengo mapya matano ya Mahakama za Wilaya za Manyoni, Kilindi, Bunda, Sikonge na Rungwe, Prof. Ole Gabriel amesema ujenzi wa jengo la Mahakama ya Manyoni limegharimu zaidi ya bilioni 1, Rungwe nalo limegharimu bilioni 1 na Mahakama ya Bunda imegharimu milioni 915.

Prof. Ole Gabriel ameongeza kuwa, Mahakama ya Wilaya ya Kilindi limegharimu limegharimu milioni 657.5 na lile la Sikonge limegharimu 601.7 na ujenzi wa majengo hayo umetumia fedha za ndani.

Ameishukuru Serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluh Hassan kwa kuendelea kuiwezesha Mahakama katika uboreshaji wa miundombinu ya majengo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Amesema watendaji wa Mahakama wataendelea kuhakikishia wanasimamia vizuri fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kuboresha miundombinu na kuongeza kuwa miradi yote inayotekelezwa watahikikisha wanaitunza na kuilinda ili iwe kutoa huduma kwa wananchi kwa muda mrefu.

Kwa upande wa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Geofrey Pinda amesema Serikali inakusudia kuanza ujenzi wa jengo la Mahakama Kuu katika Mkoa wa Singida ili kusogeza huduma hiyo kwa wakazi wa eneo hilo.

Aidha Mhe. Pinda amesema Serikali ina mpango wa kupeleka bungeni mpango wa kuboresha vyombo vinavyofanya kazi na Mahakama ili navyo viwe na mazingira mazuri ya utoaji wa huduma kwa wananchi. 

Muonekano wa moja ya majengo mapya matano yaliyozinduliwa leo tarehe 30 Januari, 2023 na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani. Jengo hili limezinduliwa kwa niaba ya majengo mapya ya Wilaya za Kilindi, Bunda, Rungwe na Sikonge.

Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa taarifa ya miradi ya Mahakama mpya za Wilaya mbele ya Mgeni rasmi ambaye alikuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani (hayupo katika picha).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni