Jumatatu, 23 Januari 2023

JAJI MKUU ATEMBELEA JENGO JIPYA LA MAKAO MAKUU YA MAHAKAMA JIJINI DODOMA.

Na Innocent Kansha - Dodoma

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ametembelea jengo jipya la Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma leo tarehe 23 Januari, 2023 na kupokelewa na mwenyeji wake Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel kisha akapata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali za kiutendaji zinazoendelea mahali hapo.

Mhe. Prof. Juma akiwa Ofisini kwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama alipata wasaa wa kupokea maelezo mafupi ya namna taratibu za ukamilishaji wa shughuli za ujenzi wa jengo hilo la makao makuu kutoka kwa mwenyeji wake Prof. Elisante Ole Gabriel.

"Nakushuru sana Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma kwa kuja leo kututembelea na kututia moyo ujio wako ni faraja kwetu sisi watumishi tunaotoa huduma katika jengo hili nimatumaini yetu shughuli zote za kiutendaji kwa watumishi wa Mahakama upande wa makao makuu zitaendelea kushamiri", alisema Prof. Ole Gabriel.  

Prof. Juma alikagua baadhi ya maeneo ikiwemo ofisi za watumishi wa Mahakama katika jengo hilo na kujionea maendeleo ya ujenzi unaendelea kukamilishwa na mkandarasi na kuridhishwa na hatua nzuri iliyofikiwa.

Jaji Mkuu Prof. Juma aliambatana na viongozi waandamizi wa Mahakama ya Tanzania ikiwa ni pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani, Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson Mdemu, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma, Msajili wa Mahakama ya Rufani Mhe. Sylvester Kahinda na Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha katika ziara hiyo fupi 

Itakubukwa kuwa Mahakama ya Tanzania imekwisha hamia Jijini Dodoma tangu tarehe 29 Disemba, 2023 katika jengo lake jipya la Makao Makuu ikiwemo baadhi ya ofisi zake za vitengo na Idara zinatoa huduma kutokea jengo hilo.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitia saini kwenye kitabu cha wageni mara alipowasili kutembelea jengo jipya la Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma leo tarehe 23 Januari, 2023 na kupokelewa na mwenyeji wake Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisalimiana na watumishi wa Mahakama wa Makao Makuu mara alipowasili kutembelea jengo jipya la Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma leo tarehe 23 Januari, 2023 na kupokelewa na mwenyeji wake Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa kwanza kulia) akiuliza jambo wakati wa ziara yake fupi ya kutembelea jengo jipya la Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma, wengine ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani (wa kwanza kulia mstari wa mbele) na  mwenyeji wa Jaji Mkuu Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati).Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani (aliyenyoosha mkono) akifafanua jambo wakati wa ziara fupi ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ya kutembelea jengo jipya la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania Jijini Dodoma.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa kwanza kushoto) akiwa kwenye mazungumzo  na mwenyeji wake Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel  alipotembelea jengo jipya la Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma leo tarehe 23 Januari, 2023. 

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa kwanza kulia) akitembezwa ndani ya jengo hilo  la Makao Makuu na mwenyeji wake Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel.
 
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa kwanza kulia) akitembezwa ndani ya jengo hilo  la Makao Makuu na mwenyeji wake Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel.
 
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa kwanza kulia) akitembezwa ndani ya jengo hilo  la Makao Makuu na mwenyeji wake Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel
 
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa kwanza kulia) akitembezwa ndani ya jengo hilo  la Makao Makuu na mwenyeji wake Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel
 
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyeinama) akimuonyesha Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma mifumo ya mawasiliano ya internet iliyowekwa ndani ya jengo hilo.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyegeukia ukutani) akimuonyesha Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma aina ya kuta za jengo sizotoa sauti nje ya chumba mtumishi awapo ofisini ndani ya jengo hilo.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa kwanza kulia) akitembezwa ndani ya jengo hilo  la Makao Makuu na mwenyeji wake Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa kwanza kulia) akitembezwa ndani ya jengo hilo  la Makao Makuu na mwenyeji wake Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa kwanza kulia) akitembezwa ndani ya jengo hilo  la Makao Makuu na mwenyeji wake Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa kwanza kulia) akitembezwa ndani ya jengo hilo  la Makao Makuu na mwenyeji wake Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitia saini kwenye kitabu cha wageni mara alipowasili kutembelea jengo jipya la Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma leo tarehe 23 Januari, 2023 na kupokelewa na mwenyeji wake Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel.

Sehemu ya Viongozi Waandamizi wa Mahakama wakisikiliza wasilisho fupi kutoka kwa Makandarasi mshauri Bi. Queen (hayupo pichani) wakati Jaji Mkuu wa Tanzania alipomtembelea Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel Ofisini kwake katika jengo la Makao Makuu ya Mahakama Jijini Dodoma, kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani (wa kwanza kushoto), Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson Mdemu (katikati) na Msajili wa Mahakama ya Rufani Mhe. Sylvester Kahinda

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akikagua sehemu ya kuta za jengo jipya la Makao Makuu ya Mahakama huku wakishudia Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani (wa kwanza kulia) na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson Mdemu (mwenye kuvalia tisherti nyeusi) 

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Esante Ole Gabriel akimuonyesha madhali ya jengo  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa pili kushoto) alipotembelea Jengo la Makao Makuu ya Mahakama Jijini Dodoma, wengine ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani (wa kwanza kulia) akitoa akifafanuzi wa jambo wakati wa ziara hiyo fupi.

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani (wa kwanza kulia) akitoa akifafanuzi wa jambo wakati wa ziara fupi ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alipotembelea Jengo la Makao Makuu ya Mahakama Jijini Dodoma, wengine ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa pili kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kulia)

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani (aliyenyoosha mkono) akitoa akifafanuzi wa jambo wakati wa ziara fupi ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alipotembelea Jengo la Makao Makuu ya Mahakama Jijini Dodoma, wengine ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa pili kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (wa kwanza kushoto), Jaji Mfawidihi Mahakama Kuu ya Tanzanmia, Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson Mdemu (mwenye tishert nyeusi) na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma (wa kwanza kulia)

Muonekano wa jengo jipya la Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma.

(Picha na Innocent Kansha Mahakama - Dodoma) Hakuna maoni:

Chapisha Maoni