Na
Innocent Kansha – Mahakama, Dodoma
Ikiwa
ni siku ya tatu toka kuzinduliwa rasmi kwa maadhimisho ya kitaifa ya wiki ya
utoaji elimu ya sheria nchini na mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango katika Viwanja vya Nyerere
Square jijini Dodoma mnamo tarehe 22 Januari, 2023, Mahakama ya Tanzania pamoja
na wadau mbalimbali wa sekta ya sheria nchini wamendelea kuwapokea wananchi na
kutoa elimu ya masuala mtambuka ya kisheria kwa wadau wa Mkoa Dodoma na viunga
vyake.
Akizungumza
wakati wa zoezi hilo la kupata elimu Bw. Iddris Haji Chukwepe mkazi wa Veyula
jijini hapa amesema, utaratibu huo wa kutenga muda maalumu na kuwapa wananchi
elimu ni mzuri sana na unalenga kupunguza malalamiko yatokanayo na ukosefu wa
elimu ya sheria na kupunguza migogoro isiyo ya lazima katika jamii.
“Binafsi
nimefurahishwa sana mimi kama mfanyabiasha mdogo (mmachinga nilivunjiwa kibanda
changu cha biashara na mgambo wa Jiji eti kwa amri ya Mkuu wa Wilaya, sikujua
nianzie wapi kudai haki yangu lakini niliposikia matangazo ya siku ya sheria, leo
nimefika banda la malalamiko la Mahakama na kuelekezwa utaratibu mzima wa namna
ya kudai mali zangu zilizopotea kwa lugha nyepesi na laini”, alieleza Bw.
Chukwepe.
Akatoa
rai kwa Muhimili wa Mahakama na wadau wa sekta ya sheria nchini kuwa elimu hiyo
yenye manufaa kwa wananchi isihishie katika wiki ya sheria bali elimu hiyo
iendelee kutolewa hasa maeneo ya vijijini waliko wananchi wengi wazalisha mali,
alisisitiza Chukwepe.
Mwananchi
huyo anatukumbusha kurejea Nukuu ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim
Hamis Juma aliyoitoa mbele ya Mgeni rasmi na Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip
Mpango siku ya uzinduzi.
Ananukuu “Ningependa kuchukua muda huu kuwaomba wananchi
ambao wanataka kudai haki zao au wanataka kufahamu haki zao, hatua ya kwanza
kabisa ya kuidai haki yako ni kuifahamu wewe mwenyewe.
"Kuifahamu
kwa kusoma, kutafuta elimu ya kuweza kukuwezesha kujua shughuli zako zinaongozwa
na sheria ipi na kwa utaratibu upi hiyo ndiyo hatua ya kwanza kabisa, kabla
hata hujamtafuta mwanasheria au ndugu na jamaa akusaidie. Wewe mwenyewe fanya
juhudi za kufahamu hizi shughuli ninazofanya zinaongozwa na sheria ipi,
zinaongozwa na utaratibu upi alafu endelea na kufanya kazi.”
Mwananchi huyo anaendelea kumnukuu Jaji Mkuu ambaye aliendea kusema, "Hii
ardhi ninayonunua inaongozwa na sheria ipi, mipaka yake ikoje kwa hiyo ukiwa
katika ufahamu huo utakuwa katika ufahamu mzuri sana utakuwa katika nafasi
nzuri sana ya kuzipigania haki zetu na vilevile kuhakikisha kwamba hiyo haki
unaipata kwa urahisi zaidi.”.
Mdau wa Mahakama
ya Tanzania akielezea jambo alipotembelea banda la Kituo cha Usuluhishi cha Mahakama Kuu ya Tanzania leo tarehe 24 Januari, 2023 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Mdau wa Mahakama ya Tanzania akipokea ufafanuzi wa jambo alipotembelea banda la Kituo cha mawasiliano cha huduma kwa mteja leo tarehe 24 Januari, 2023 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Mdau wa Mahakama ya Tanzania akisaini kitabu cha wageni alipofika kupata huduma katika Banda la Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) lushoto.
Wadau wa Mahakama ya Tanzania wakifafanuliwa jambo na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kituo cha Usuluhishi, Mhe. Wanje Hamza walipotembelea banda la Kituo cha Usuluhishi cha Mahakama Kuu ya Tanzania leo tarehe 24 Januari, 2023 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Wadau wa Mahakama ya Tanzania wakipewa ufafanuzi wa jambo walipotembelea banda la Mirathi la Mahakama ya Tanzania.
Wadau wa Mahakama ya Tanzania wakipatiwa maelekezo walipotembelea banda la Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Kituo katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Wadau wa Mahakama ya Tanzania akielezea jambo walipotembelea banda la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Jijini Dodoma katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Wadau wa Mahakama ya Tanzania wakisiliza maelezo kutoka kwa wataalu wa Mabaraza ya ardhi nchini walipotembelea banda la Mabaraza ya ardhi na Usuluhishi.
Sehemu ya wadau wa Mahakama ya Tanzania walipotembelea banda la Wizara ya Katiba na Sheria wakimsikiliza mtaalu kutoka wizara hiyo katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Mdau wa Mahakama ya Tanzania akielezea jambo alipotembelea banda la Usimamizi wa mashauri Mahakama ya Tanzania akisikilizwa na Mkurugezi wa kurugenzi ya usimamizi wa mashauri wa mahakama ya Tanzania, Mhe. Desidery Kamugisha (kushoto) katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Wadau wa Mahakama ya Tanzania wakisiliza ufafanuzi wa jambo kutoka kwa wataalum kituo cha sheria na haki za binadamu walipotembelea banda hilo katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Wadau wa Mahakama ya Tanzania wakiuliza jambo kutoka kwa wataamu wa Taasisi ya Usalama Mahala pa Kazi walipotembelea banda la Kituo hicho katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Wadau wa Mahakama ya Tanzania wakimsikiliza mtaamu walipotembelea banda la kutoa elimu katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Wadau wa Mahakama ya Tanzania wakipewa ufafanuzi walipotembelea banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Mhe. Burhan Mohamed akielezea jambo alipotembelewa na wadau wa Mahakama katika banda la Kituo cha Usuluhishi cha Mahakama Kuu ya Tanzania leo tarehe 24 Januari, 2023 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Mdau wa Mahakama ya Tanzania akipokelewa katika banda la mapokezi tayari kwa kutembelea mabanda ya kutoa elimu katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Mtaalamu kutoka katika kitengo cha maboresho ya Mahakama ya Tanzania akielezea jambo alipotembelewa na wadau wa Mahakama katika banda hilo leo tarehe 24 Januari, 2023 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Wadau wa Mahakama ya Tanzania wakipata maelezo kutoka kwa wataamu wa Idara ya Huduma za Uangalizi walipotembelea banda hilo katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Wadau wa Mahakama ya Tanzania wakisubiria kupata huduma katika bada la RITA katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Mdau wa Mahakama ya Tanzania akielezea jambo alipotembelea banda la Kituo cha Mawasiliano kwa mteja cha Mahakama ya Tanzania katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Picha na Innocent Kansha - Mahakama
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni