Jumatano, 4 Januari 2023

JAJI MKUU AUNGANA NA WANAFAMILIA KUOMBOLEZA KIFO CHA JAJI DKT. JONH UTAMWA

Na Mwandishi wetu

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma leo tarehe 4 Januari, 2023 ameungana na waombolezaji wengine wakiwemo wanafamilia, majirani, Watumishi wa Mahakama ya Tanzania, Viongozi mbalimbali wa Serikali, Kijamii, Kidini na wakaazi wa eneo la Madale-Tegeta  jijini Dar es salaam kuomboleza kifo cha aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Iringa, Mhe. Dkt. John Utamwa nyumbani kwake.

Mwili wa marehemu Jaji Dkt. Utamwa uliwasili nyumbani kwake majira ya saa tisa (9) alasiri ukitokea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ulikokuwa umehifadhiwa. Mara baada ya kuwasili nyumbani kwake ilifanyika ibada fupi ya kumuombea marehemu kwa Mungu kwa taratibu za dini ya Kikristo.

Kisha Mwili utapumzishwa nyumbani kwake Madale-Tegeta jijini Dar es Salaam kutoa fursa kwa wapendwa wake kuuaga kifamilia hadi kesho tarehe 05 Januari Mwaka huu, kupisha taratibu za kuagwa rasmi Kiserikali hapo kesho katika Kanisa la Mtakatifu Alban la kianglikana Posta Jijini Dar es salaam.

Baada ya taratibu zote kukamilika mwili unatarajiwa kusafirishwa kwa ajili ya mazishi Siku ya Jumamosi, tarehe 07 Januari, 2023 katika Kijiji cha Msemembo kilichopo Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa heshima kwa mwili wa marehemu Mhe. Dkt. John Utamwa aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Iringa nyumbani kwake Madale -Tegeta Jijini Dar es salaam, alipoungana na waombolezaji wengine kuomboleza msiba huo leo tarehe 4 Januari, 2023.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa pole kwa mjane wa marehemu Mhe. Dkt. John Utamwa aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Iringa nyumbani kwake Madale -Tegeta Jijini Dar es salaam, alipoungana na waombolezaji wengine kuomboleza msiba huo.


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisaini kwenye kitabu cha maombolezo alipoungana na waombolezaji wengine kuomboleza msiba wa marehemu Mhe. Dkt. John Utamwa aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Iringa nyumbani kwake Madale -Tegeta Jijini Dar es salaam.

Sehemu ya Watoto wa marehemu Mhe. Dkt. John Utamwa aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Iringa wakiwa kwenye majonzi nyumbani kwao Madale -Tegeta Jijini Dar es salaam. 

Mjane wa marehemu Mhe. Dkt. John Utamwa (aliyeketi katikati) akifalijiwa na majirani zake wakati wa maombolezo nyumbani kwake Madale -Tegeta Jijini Dar es salaam

Geneza lililobeba Mwili wa marehemu Jaji Dkt. Utamwa ukiwa nyumbani kwake.



Sehemu ya waombolezaji walioungana na Mjane wa Marehemu wakishuhudia Geneza lililobeba Mwili wa marehemu Jaji Dkt. Utamwa ukiwa nyumbani kwake.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa kwanza kushoto) akiwa msibani na sehemu ya Majaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania waliofika kuomboleza msiba huo.


Sehemu ya Majaji wa Mahakama ya Kuu ya Tanzania waliofika kuomboleza msiba hapo.

Mjane wa marehemu Jaji Dkt. Utamwa (aliyekati katikati) akiwa na sehemu ya watoto wake wakati wa ibada fupi ya kumuombea marehemu nyumbani kwake.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa tatu kushoto) akishudia geneza lililobeba Mwili wa marehemu Jaji Dkt. John Utamwa akiwa na sehemu ya Majaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na baadhi ya ndugu waliofika kuomboleza msibani hapo.


Sehemu ya Waombolezaji waliofika nyumbani kwa marehemu Jaji Dkt. John Utamwa.

Sehemu ya Waombolezaji waliobeba Geneza lenye mwili wa marehemu Jaji Dkt. John Utamwa ulipowasili nyumbani kwake.




Sehemu ya Waombolezaji waliofika nyumbani kwa marehemu Jaji Dkt. John Utamwa.


Sehemu ya Waombolezaji waliofika nyumbani kwa marehemu Jaji Dkt. John Utamwa.
 

Mchungaji akitoa nasaa wakati wa ibada fupi ya kumuombea marehemu Jaji Dkt. John Utamwa nyumbani kwake.



Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa tatu kutoka kulia) akishiriki Ibada fupi ya kumuombea marehemu Jaji Dkt. John Utamwa wakati wa maombolezo hayo, wengine ni sehemu ya Majaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania.

(Picha na Innocent Kansha - Mahakama)



 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni