Na
Magreth Kinabo-Mahakama
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi. Mhe. Agnes Mgeyekwa leo tarehe 26 Januari, mwaka 2023 amewaongoza majaji wa Mahakama hiyo kutoa elimu ya usuluhishi ili kuweza kutatua migogoro ya ardhi kwa njia hiyo.
Jaji huyo aliambatana na
majaji wenzake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam kwa
ajili ya kutoa elimu hiyo, na kuweza kuzungumza na baadhi ya wananchi ambapo
Wiki ya Sheria inapoadhimishwa.
Akizungumza na waandishi
wa habari, kwa niaba ya majaji wenzake, Jaji wa Mahakana Kuu ya Tanzania Divisheni
ya Ardhi, Mhe. Dkt. Benhaji Masoud alisema
wanatoa elimu hiyo ili kuweza
kutatua migogoro ya ardhi kabla ya kufika mahakamani, kwa kuwa hivi sasa
migogoro hiyo inafanyiwa usuluhishi baada ya kufika mahakamani.
“Utatuzi wa migogoro ya
ardhi kwa njia hiyo ni unaokoa gharama, muda, kudumisha mahusiano na kukuza
uchumi. Hivyo usuluhishi ni njia pekee ya kutatua migogoro ya ardhi,” alisema
Jaji Masoud.
Alitoa wito kwa wananchi
kutumia njia ya usuluhishi, kwa kuwa ni vigumu kuzaa mgogoro mwingine. Jaji
Masoud aliowaomba wananchi kufika katika banda ya Mahakama Kuu ya Tanzania
Divisheni ya Ardhi ili kuweza kupata uelewa wa utumiaji wa njia hiyo, ikiwa ni
hatua ya kuwawezesha kushiriki katika shughuli za uzalishali mali na kukuza
uchumi.
Baadhi ya wananachi
waliopata elimu hiyo, waliwaomba wananchi wenye migogoro ya ardhi kufika katika
banda hilo ili kuweza kuelimishwa njia sahihi ya kutatua suala hilo.
Mahakama hiyo kwa kipindi
cha mwaka 2021 ilibakia na mashauri 1,591 mwaka 2022 ilisajili mashauri 2,111 kwa
njia ya mtandao, mashauri yaliyoamriwa ni 2,768 sawa na asilimia 131 na
yanayoendelea ni 934.
Wiki hiyo ilianza kuadhimishwa Januari 22, mwaka 2023 hadi Januari 29, mwaka 2023 huu yenye kauli mbiu ya “Umuhimu Wa Utatuzi wa Migogoro kwa Njia ya Usuluhishi Katika Kukuza Uchumi Endelevu.”
Kanali Mstaafu Merikiori
Mtega (kushoto) akipata elimu kuhusu utumiaji wa njia ya usuluhishi katika
kutatua migogoro ya ardhi kutoka kwa mahakama hiyo leo, kwenye viwanja vya
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kutoka (kushoto wa pili) ni Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi. Mhe. Agnes Mgeyekwa,
wa (kwanza kushoto) ni mhe. Jaji Dkt.Theodora Mwenegoha. (Kulia wa pili) ni Mhe. Jaji
Dkt. Benhaji Masoud na wa kwanza kulia ni Mhe Jaji Kevin Mhina.
Gratiana
Rwakibarila (kushoto) akipata elimu kuhusu utumiaji wa njia ya usuluhishi
katika kutatua migogoro ya ardhi kutoka kwa mahakama hiyo leo, kwenye viwanja
vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kutoka (kushoto wa pili) ni Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi. Mhe. Agnes Mgeyekwa,
wa (kwanza kushoto) ni mhe.Jaji Dkt.Theodora Mwenegoha. (Kulia wa pili) ni Mhe. Jaji
Dkt. Benhaji Masoud na wa kwanza kulia ni Mhe Jaji Kevin Mhina.
Hamis
Kipande (kulia) na Ismail Omary wakipata elimu kuhusu utumiaji wa njia ya
usuluhishi katika kutatua migogoro ya ardhi kutoka kwa mahakama hiyo leo,
kwenye viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam. (wa kwanza kushoto) ni mhe. Jaji Dkt.Theodora
Mwenegoha. (katikati) ni Mhe. Jaji Dkt. Benhaji Masoud na kulia
ni Mhe Jaji Kevin Mhina.
“
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni