Ijumaa, 27 Januari 2023

MWENYEKITI WA BARAZA LA USHINDANI ATEMBELEA MAONESHO WIKI YA SHERIA DODOMA

Na Tiganya Vincent-Mahakama, Dodoma

Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (FCT) ambaye pia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe.  Salma. Maghimbi leo tarehe 27 Januari, 2023 ametembelea mabanda mbalimbali ya maonesho wa Wiki ya Sheria yanayoendelea kutoa elimu kwa wananchi.

Akiwa katika viwanja vya Nyerere Square jijini hapa, Mhe. Maghimbi amepata fursa kutembelea mabanda ya Jeshi la Polisi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraza la Ushindani, Kituo cha Utoaji Taarifa cha Mahakama ya Tanzania, Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) na Taasisi ya Kuzuia na KUpambana na Rushwa.

Mabanda mengine ni Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni, Mahakama ya Afrika Mashariki na Kituo cha Usuluhishi cha Mahakama Kuu ya Tanzania. Ifuatayo ni habari katika picha katika ziara hiyo:

Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (FCT) ambaye pia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi (kulia) akitoa ushauri kwa mtumishi wa Mahakama ya Afrika Mashariki wakati alipotembelea banda lao kwenye maonesho ya Wiki ya Sheria leo tarehe 27 Januari 2023 yanayoendeleo katika Viwanja vya Nyerere Squares jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza laUshindani (FCT) ambaye pia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi (kushoto) akimsikiliza Naibu Msajili katika Kurugenzi ya Huduma za Kimahakama Ukaguzi na Maadili, Mhe. Kinabo Minja (kulia)alipotembelea banda hilo.
Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (FCT) ambaye pia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi (kulia) akiangalia machapisho mbalimbali alipokuwa katika Banda la Chama cha Mawakili cha Tanganyika (TLS).

Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (FCT) ambaye pia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi (kulia) akitoa ushauri kwa wanachama wa Chama cha Majaji wanawake nchini (TAWJA) wakati alipotembelea banda lao la maonesho ya Wiki ya Sheria 2023.

Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (FCT) ambaye pia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi (kulia) akitoa ushauri kwa watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa. 

Mwenyekiti wa Baraza laUshindani (FCT) ambaye pia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi (kulia) akitoa ushauri kwa Mzee Gideon Kazeni (kushoto) wakati alipotembelea maonesho ya Wiki ya Sheria leo tarehe 27 Januari 2023.

(Picha na Tiganya Vincent) 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni