Jumamosi, 28 Januari 2023

TANZIA; MTUMISHI WA MAHAKAMA YA WILAYA SAME AFARIKI DUNIA

Katika picha ni Bw. Aloyce Mbonea enzi za uhai wake.

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake aliyekuwa Msaidizi wa Kumbukumbu katika kituo cha kazi cha Mahakama ya Wilaya ya Same, Bw. Aloyce Mbonea kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 28 Januari, 2023 .

Kwa mujibu wa Mtendaji wa Mahakama Kuu-Kanda ya Moshi, Bw. Donald Makawia  marehemu Mbonea alikutwa na umauti katika Hospitali ya 'KCMC' alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari iliyotokea tarehe 30 Desemba, 2022. 

Taratibu za maziko zinaendelea kufanyika. 

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.

 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni