Na Magreth Kinabo
–Mahakama Tanga
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesema kwamba Bunge liko tayari kubadili sheria zinazoleta changamoto katika mashauri yanayohusu ukatili wa kijinsia hususan kwa wanawake ,watoto na watu wenyeulemavu.
Akizungumza katika
mkutano wa siku mbili wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) ambapo alikuwa mgeni rasmi
kwa niaba ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan unaofanyika kwenye hoteli ya New Tanga Beach Resort alikishauri chama
hicho kuangalia namna ya kutoa haki kwa makaundi hayo.
“Utakuta mtoto amefanyiwa kitendo cha ukatili wa kijinsia na
mtuhumiwa amekamatwa baada ya sisikujiridhisha, halafu anaachiwa sasa
tunajiuliza kama mtuhumiwa ameachiwa nani ametenda kitendo hicho na mtoto na ameathirika,
lakini hatuambiwi nani ametenda kosa hilo. Kama sheria zinazotumika ni
changamoto sisi tuko tayari kubadilisha, ili haki iweze kutendeka,” alisema
Spika Tulia.
Aliongeza kwamba kuwa
ni lazima jamii ikapewa elimu kuhusu uendeshaji wa
mashauri yanayohusu makundi hayo ili iwe salama nayi pia muwe salama na kila mtu
awe na amani katika uendeshaji wa
mashauri hayo.
Spika Tulia alisema kuwa wanachama wa TAWJA wanapotaoa hukumu
anu maamuzi ya ukatili wa kijinsia watoe haki inayozingatia usawa na wakati ili
mtu asione kuwa ametendewa haki kwa kutokana umasikini , mwanamke, mtoto au ni
mtu mwenye ulemavu.
“Mafanikio yenu hayapimwi kwa kuzingatia hukumu au maamuzi
yaliyoandikwa, idadi ya vikao vya maamuzi na idadi ya mizozo, bali yanapimwa
kwa namna gani tafsiri ya hukumu au maamuzi hayo yanatoa nafasi kwa
jamii kuweza kuondokana na ubaguzi na ukatili wa kijinsia,“ hivyo ni wakati wa
wao kusimama imara na kutekeleza
majukumu yao ,”alisisitiza.
Aidha Spika huyo alisema kuwa wanachama 20 waliopatiwa
mafunzo kuhusu suala hilo la namna ya kuendesha mashauri ya ukatili wa kijinsia
wayatumie, kuboresha utendaji kazi, huku akisisitiza kwamba ni vizuri wanachama
wanaopatiwa mafunzo wangalie kuwa mtu ana mchango gani au anatetea nini.
Aliwataka wanachama hao, kutumia wakati huo muhimu kwenye
mkutano huo kujadili kuhusu Mpango Mkakati wa mwaka 2023 na kuchagua viongozi
wenye sifa ya kukipeleka mbele chama hicho na kutekeleza malengo yake.
Aliwaasa kuendelea kuwa na maadili mema ili kuweza kuendelea
kujenga heshima na kujenga Imani kwa wananchi.
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.Prof Ibrahim Hamis
Juma alisema ni lazima uongozi wa TAWJA uweke utaratibu wa kuweka kumbukumbu na
kutangaza mafanikio yanayotokana na kazi mbalimbali zinazofanywa na wanachama,
ikiwemo michango mingi ya kujitolea
ambayo wanachama wameitoa.
Jaji Mkuu huyo alitoa
takwimu za mhimili huo za Desemba
31,mwaka jana ambazo zinaonyesha uwepo wa wanachama wa TAWJA kila kona ya
Mahakama, akianzia idadi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani kuwa ni 26 ambapo kati
ya hao wanaume ni 16 sawa na asilimia 62
na wanawake ni 10 sawa na asilimia 62. Idadi ya Mahakama Kuu ni 97, Majaji
wanaume ni 62 sawa na asilimia 64 na wanawake ni 35 sawa na asilimia 36.
Aliongeza kuwa idadi
ya Majaji Wafawidhi ni 24, wanaume ni 16 sawa na asilimia 67 na wanawake ni nane
sawa na asilimia 33. Wasajili ni watatu, wanaume ni wawili sawa na asilimia 67 na
wanawake ni mmoja sawa na asilimia 33, Naibu Wasajili ni 53, wanaume ni 33 sawa
na asilimia 62, wanawake ni 20 sawa na asilimia 38. Idadi Ya Mahakimu Wakazi Mahakama
za Mahakama za Hakimu Mkazi ni 69, wanaume ni 38 sawa na asilimia 55 na
wanawake ni 31 sawa na asimilia 45.
Idadi ya Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama za Hakimu
Mkazi ni 28. Idadi ya Mahakimu Wakazi wa Mahakama za Wilaya ni 284 ,wanaume ni
141 sawa na asilimia 50 na wanawake ni 143 sawa na asilimia 59. Idadi ya
Mahakimu wakazi wa Mahakama za Wilaya ni 135, wanaume ni 76 sawa na asilimia 56
na wanawake ni 59 sawa na asilimia 44. Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo ni 875,
wanaume ni 408 sawa na asilimia 47 na wanawake ni 467 sawa na asilimia 53,
wengine Mahakimu Wafawidhi wa Mahakama
za Mwanzo ni 577, wanaume ni 329 na wanawake ni 248.
“Ni muhimu zaidi kwa kila mwanachama atatumiaje uwepo wake kwa
uchache wenu katika kutatua usawa wa
kijinsia na uwezeshwaji wa wanawake ili nao wafaidiMaendeleo Endelevu na
wafurahie Haki za Binadamu,”alisisitiza Jaji Mkuu huku akiwashauri kuendelea kujifunz
na kufanya tafiti.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis
Ramadhani Abdalla,ambaye alisema ataendele kuwa na ushirikiano na chama hicho na
kuongeza kwamba Zanzibar ina Majaji 12
kati yao wanne ni wanawake na Mahakimu 64 , ambapo wanawake ni 23.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Omary Mgumba aliomba vyombo vya
usafiri vinavyokamatwa katika biashara haramu vishikiliwa, akiwemo mtuhumiwa
hadi kesi itakapoisha.
Naye Mwenyekiti ws Chama
cha TAWJA ambaye pia ni Jaji
Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Joaquine De Mello alisema chama hicho
ina wanachama 300.
Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akitoa hotuba ya ufunzi wa mkutano wa siku mbili wa
Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) unaofanyika katika hoteli
ya New Tanga Beach Resort.
Jaji Mkuu wa
Tanzania, Mhe. Ibrahim Hamis Juma akitoa hotuba yake katika mkutano huo.
Jaji Mkuu wa Zanzibar,
Mhe. Khamis Ramadhani Abdalla akizungumza jambo katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha TAWJA ambaye pia ni Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Joaquine De Mello akizungumza jambo kwenye mkutano huo.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Omary Mgumba akizungumza jambo.
Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, (katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki katika mkutano huo. Wa pili kulia ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.
Ibrahim Hamis Juma wa kwa pili (kulia) na wa kwanza (kushoto) ni ni Jaji Mkuu
wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhani Abdalla, wa pili kulia ni Mwenyekiti wa
Chama cha TAWJA ambaye pia ni Jaji Mstaafu wa
Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Joaquine De Mello na wa kwanza (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Omary Mgumba.
Meza kuu ikisikiliza mada.
Jaji Mstaafu wa
Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sophia Wambura akisisitiza jambo.
Jaji wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, Mhe. Leila Mgonja, akichangia hoja.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanjelwa Mbeya, Mhe. Angela Byera akichangia hoja katika mkutano huo.
(Picha na Magreth Kinabo - Mahakama)
da
.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni