Marehemu Nicolaus Mgeta Rumbe enzi za uhai wake.
Mahakama ya
Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Bw. Nicolaus
Mgeta Rumbe (katika picha) aliyekuwa Mtumishi wa Mahakama ya Mwanzo Nyambono iliyoko Wilayani
Musoma.
Kwa mujibu wa
Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, Bw. Festo Chonya marehemu Rumbe alifikwa
na umauti tarehe 23/02/2023 kutokana na ugonjwa wa kisukari.
Mazishi
yake yamefanyika leo tarehe 25/02/2023 katika kijiji cha Bugoji kilichopo
Musoma Vijijini.
Marehemu Nicolaus
Mgeta Rumbe alizaliwa 12/07/1966 na kuajiriwa katika Mahakama ya Tanzania
tarehe 16/04/1984.
Mahakama ya
Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza katika kipindi hiki
kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni