Jumanne, 21 Februari 2023

‘UTATUZI WA MIGOGORO YA KAZI KWA WAKATI CHACHU KWA MAENDELEO YA TAIFA’

Na. Stanslaus Makendi na Arapha Rusheke-Mahakama, Dodoma 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson Mdemu amesisitiza kuwa utatuzi wa migogoro ya kazi kwa kuzingatia taratibu za kisheria na muda ni chachu kwa maendeleo ya taifa.

Mhe. Mdemu aliyasema hayo hivi karibuni wakati anafungua mafunzo ya Wasuluhishi na Waamuzi wa mashauri ya kazi nchini yanayoendelea katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Dodoma. Mafunzo hayo yanafanyika kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 20 hadi 24 Februari, 2023. 

Jaji Mfawidhi huyo alibainisha kuwa upo umuhimu mkubwa wa kutatua migogoro ya kazi kwa wakati ili kuleta manufaa katika maisha ya mtu mmoja mmoja na hatimaye faida kwa taifa. Sambamba na hilo, aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kutumia fursa hiyo kubadilishana uzoefu ili kuboresha zaidi dhana ya usuluhishi nchini. 

Aliongeza kuwa, utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi ni takwa la kikatiba na njia rahisi ya kutafuta suluhu ya migogoro nje ya mfumo rasmi wa uendeshaji wa mashauri husika mahakamani. 

Kadhalika, aliwataka washiriki kutambua kuwa Mahakama ya Tanzania imejielekeza huko katika kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi, ndio maana kauli mbiu ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria mwaka huu 2023 inahamasisha utatuzi wa migogoro kwa njia hiyo. 

Jaji Mfawidhi huyo aliinukuu kauli mbiu hiyo ionayosema, “Umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu; Wajibu wa Mahakama na wadau,” na kuwataka wadau kila mmoja wao kutimiza wajibu wake. 

Alibainisha kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwakutanisha Mahakama na wadau muhimu katika mashauri ya kazi kwa lengo la kuwajengea uwezo katika uendeshaji wa mashauri ya kazi na utoaji wa tuzo. 

Mhe. Mdemu alieleza kwamba mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Mafunzo ya Mahakama ya Tanzania, 2019 sambamba na utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama (2021/2022 – 2024/2025) kwa lengo kubwa la kuboresha huduma za Mahakama. 

Aliwahimiza wote kushiriki kikamilifu katika mafunzo hayo ili lengo lake liweze kufikiwa kama ilivyokusudiwa, hivyo ana imani kupitia mada mbalimbali zitakazowasilishwa na wawezeshaji wenye maarifa na weledi zitawapa maarifa ambayo yatawasaidia kutekeleza majukumu yao.

Mafunzo hayo ya siku tano yameandaliwa na Mahakama ya Tanzania na yanahusisha Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Wasaidizi wa Sheria wa Majaji, Mwenyekiti, Makamishna, Mtendaji Mkuu, Wakurugenzi, Wasuluhishi na Waamuzi kutoka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).

 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson Mdemu (aliyesimama) akitoa neno la ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Dodoma.

Sehemu ya washiriki na wadau wa Mahakama wakifuatilia mafunzo hayo.

 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson Mdemu (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo. Walioketi kuanzia kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Uamuzi na Usuluhishi, Bw. Edris Mavula, Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mhe. Biswalo Mganga, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina, Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Modesta Opiyo Makopolo, Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mhe. Katarina Mteule  na Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Kazi.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson Mdemu (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo. Walioketi kuanzia kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Uamuzi na Usuluhishi, Bw. Edris Mavula, Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mhe. Biswalo Mganga, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina, Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Modesta Opiyo Makopolo, Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mhe. Katarina Mteule  na Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Kazi.Waliosimama ni Naibu Wasajili na Watendaji wa Mahakama .

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe.Gerson Mdemu (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wote wa mafunzo hayo.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson Mdemu (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo. Walioketi kuanzia kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Uamuzi na Usuluhishi, Bw. Edris Mavula, Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mhe. Biswalo Mganga, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina, Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Modesta Opiyo Makopolo, Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mhe. Katarina Mteule  na Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Kazi.
(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni