Na Magreth
Kinabo-Mahakama
Jaji Kiongozi wa Mahakama
Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani kesho tarehe 3 Machi, 2023 anatarajiwa
kufunga kikao kazi cha cha
mapitio ya bajeti ya nusu ya mwaka 2022/23 na uchambuzi wa maandalizi ya bajeti ya mwaka 2023/24 ya Mahakama ya Tanzania.
Kikao hicho kilianza tarehe tarehe 27 Februari 2023 kinachoendelea
Jijini Dodoma, ambapo lengo lake ni
kufanya mapitio ya kina ya utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2022/23 na kuchambua
mipango ya maandalizi ya bajeti ya mwaka 2023 /24 ya Mahakama hiyo.
Akizungumzia kuhusu kikao hicho, Mkurugenzi
wa Mipango na Ufuatiliaji, Bw.Erasmus Uisso alisema kinaenda vizuri na kinamalizika leo tarehe 2
Machi, 2023 kwa mujibu wa ratiba. Hivyo kila kanda ya Mahakama na Divisheni
imejiandaa vizuri.
‘‘Katika kikao hiki
kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 eneo la usikilizaji wa mashauri
limepewa kipaumbele ili liweze kuwa na bajeti ya kutosha,’’ alisema Uisso.
Aliongeza kwamba kupitia
maandalizi ya bajeti ya mwaka 2023/24 kanda za Mahakama zimewasilisha mahitaji
ya nyongeza kwa sababu ya uanzishaji wa mahakama za wilaya mpya na uanzishaji
wa Mahakama Kuu Kanda ya Manyara. Pia alisema mahitaji bajeti ya nyongeza imetokana
na mpango wa kuanzisha Mahakama Kuu Kanda ya Geita inayotajiwa kuanza kufanya kazi Julai, mwaka 2023.
Mkurugenzi huyo
aliishukuru Serikali kwa mgawo wa fedha ambao iliutoa kwa kila ngazi ya
Mahakama kama ilivyopangwa kwa ajili ya kutekeleza majukumu mbalimbali.
Aidha Uisso alisema bado
Mahakama hiyo inakabiliwa na changamoto ya mahitaji ya vitendea kazi, magari,kompyuta
na uhaba wa watumishi.
Mwenyekiti wa kikao kazi cha mapitio ya bajeti ya nusu mwaka 202/23 na uchambuzi wa maandalizi ya bajeti ya mwaka 2023/24 ya Kituo Jumuishi cha Masuala ya Kifamilia,Bw.Leonard Magacha akiongoza kikao hicho leo kinachoendelea Jijini Dodoma.
Mjumbe wa kikao hicho, Mhe. Sharmillah Sarwatt (kulia) akizungumza jambo kuhusu bajeti hiyo. Anayefuatia ni mjumbe wa kikao hicho, Bw.Joseph Elikana.
Mtendaji
wa ya Kituo Jumuishi cha Masuala ya Kifamilia, Bi. Mary Shirima wa (pili kushoto)
akifafanua jambo kwenye kikao hicho, wengine (wa mwisho kushoto)ni Naibu
Msajili wa kituo hicho Mhe. Martha Mpaze na watatu kutoka kushoto ni Leornard
Kilala ambaye ni Afisa Tawala na (kwanza kushoto) ni Mkaguzi wa Ndani,Bw,
Mujaya Mujaya wote kutoka kituo hicho.
Wajumbe kutoka Mahakama Kuu ya Tabora (walioketi kulia) wakiwasilisha mapitio ya bajeti yao, na walioketi (kushoto katikati) ni jopo la kikao hicho likiongozwa na Mwenyekiti wa kikao kazi hicho Godfrey Mashafi, (aliyeketi katikati mbele)ni Katibu wa jopo hilo, Bi. Zawadi Ngonde.
Wajumbe wa kikao hicho kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya wakiwasilisha mapitio ya bajeti yao wa (kwanza kushoto mwenye shati la damu ya mzee)ni Mtendaji wa Kanda hiyo Bw. Teofard Ndomba(katikati) ni Naibu Masajili wa Kanda hiyo, Mhe. Projesta Kahyoza na (tatu kushoto)ni Afisa Bajeti, Bw.Joseph Namiata.
Mwenyekiti wa Kikao hicho cha bajeti ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Dkt. Angelo Rumisha akizungumza jambo na (kulia) ni mjumbe wa kikao hicho, Mhe. Kinabo Minja akifuatilia mapitio ya bajeti ya kanda hiyo.
Wajumbe wa kikao hicho kutoka Mahakama wakiendelea kuhitimisha kazi hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni