Na Francisca Swai-Mahakama, Musoma.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe.
Marlin Komba amewaasa viongozi wa Mahakama katika Wilaya ya Serengeti kuwa na
mipango madhubuti inayozingatia vipaumbele katika kuboresha mazingira ya kazi.
Mhe.
Komba alitoa wito huo hivi karibuni akiwa katika ziara ya kukagua shughuli za
kimahakama wilayani Serengeti. Aliwasisitiza kujiwekea mipango ya muda mrefu na
muda mfupi inayotekelezeka kwa kuzingatia rasilimali zilizopo na uhalisia wa
uwezo wa kifedha ili shughuli zisikwame.
Kadhalika,
Mhe. Komba aliwahimiza viongozi hao kuboreshaji wa mazingira ya kazi, jambo
linalochangia kuongeza morali kwa watumishi na kujenga heshima ya Mahakama
katika jamii.
Kwa
upande wao, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Musoma, Mhe. Frank Moshi na
Mtendaji wa Mahakama wa Kanda, Bw. Festo Chonya waliwapongeza watumishi wa
Serengeti kwa kasi nzuri ya usikilizaji wa mashauri na kuwasihi kuwa makini na
ukusanyaji wa maduhuli ili kuhakikisha fedha ya Serikali hazipotei.
Mlinzi
wa Mahakama ya Mwanzo Ngoreme, Bw. Chacha Maro (aliyesimama) akiushukuru
uongozi wa Mahakama Kuu Musoma kwa ujenzi wa jengo la Mahakama hiyo, jambo
lililowaletea heshima watumishi wa Mahakama hiyo baada ya kupata jengo jipya la
kisasa.
Jaji
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Marlin Komba (katikati),
Naibu Msajili Mhe. Frank Moshi (wa tatu kulia), Mtendaji wa Mahakama, Bw Festo
Chonya (wa pili kulia), Hakimu Mkazi Mfawidhi Serengeti Mhe. Jacob Ndira (wa
tatu kushoto), Afisa Tawala Serengeti, Bi. Faraja Barakazi (wa kwanza kushoto)
wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Ngoreme.
Wegine ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Ngoreme, Mhe. Peter Malima (wa kwanza kulia)
na Bw. Chacha Nsaho Mlinzi wa Mahakama hiyo (wa pili kushoto).
Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Natta anayetembelea Mahakama ya Mwanzo
Kenyana, Mhe. Rogate Manjuu (aliyesimama) akisoma taarifa ya utendaji kazi wa
Mahakama ya Mwanzo Kenyana.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Mugumu Mjini, Mhe. Felix Ginene akisoma
taarifa ya utendaji kazi wa kituo hicho mbele ya Mhe. Komba (hayupo pichani),
viongozi na watumishi wa Mahakama hiyo.
Jaji
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Marlin Komba akielezea jambo
katika ubao wa ada na tozo mbalimbali za Mahakama alipotembelea Mahakama ya
Mwanzo Mugumu Mjini.
Jaji
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Marlin Komba (katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watumishi wa Mahakama ya Mwanzo
Mugumu Mjini.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Serengeti, Mhe. Jacob Ndira (aliyesimama)
akisoma taarifa ya utendaji kazi wa Mahakama hiyo mbele ya Mhe. Komba pamoja na
watumishi.
Jaji
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Marlin Komba (katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Serengeti.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Mwanzo Robanda, Mhe. Akinyi Mlowa (aliyesimama)
akisoma taarifa ya utendaji kazi mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania,
Kanda ya Musoma, Mhe. Marlin Komba na viongozi alioambatana nao.
Jaji
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Marlin Komba na viongozi
wakiwa katika picha ya pamoja na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo
Natta, Mhe. Rogathe Manjuu (wa pili kulia) mbele ya jengo la Mahakama ya Mwanzo
Natta.
Mahakama
ya Mwanzo Ngoreme kabla (juu) na baada ya ukarabati (chini).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni