Jumatano, 1 Machi 2023

MATUKIO KATIKA PICHA YA UCHAMBUZI WA BAJETI

Mkurugenzi wa Mipango na Ufuatiliaji wa Mahakama ya Tanzania, Bw.Erasmus Uisso akitoa maelezo kwa wajumbe wa bajeti wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba  katika kikao cha mapitio ya bajeti ya nusu mwaka 2022/23 na uchambuzi wa bajeti ya 2023/24 kinachoendelea jijini Dodoma.

Wajumbe wa bajeti wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba  wakiwa  katika kikao cha mapitio ya bajeti ya nusu mwaka 2022/23 na uchambuzi wa bajeti ya 2023/24 kinachoendelea jijini Dodoma. wa (kwanza kushoto) ni Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Bw.Lothan  Simkoko (katikati)ni Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Mhe.Odira Amworo na kulia ni  Afisa Bajeti, Bw.Mushobozi Nsangila,

Mjumbe wa kikao hicho, Mhe. Charles  Magesa (katikati kulia) akichangia hoja kwenye kikao hicho katika bajeti ya Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Mtwara.

Wajumbe wa kikao hicho kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara wakisikiliza maelezo yao kuhusu bajeti hiyo, wa (kwanza kushoto aliyevaa suti)ni Mtendaji wa Mahakama hiyo, Bw. Richard  Mbambe, (katikati) ni Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Mhe. Fredrick Lukuna na anayefuatia ni Afisa Bajeti, Bw. Zabron Zebadayo.

 Mwenyekiti wa Kikao hicho cha bajeti ya Mahakama Kuu ya Tanzania ,Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Dkt. Angelo Rumisha na mjumbe wa kikao hicho, Mhe. Kinabo Minja wakifuatilia bajeti ya Mahakama hiyo.

Mtendaji wa Mahakama Kuu  ya Tanzania,Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Bi. Masalu Kisasila(kushoto) akiwasilisha bajeti ya Mahakama hiyo na kulia ni Afisa Bajeti, Bi. Joyce Mulugu.

Jopo la kikao hicho likichambua bajeti ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu likiongozwa na Mwenyekiti, Bw. Godfrey Mashafi na Katibu  wake ni Bi. Zawadi  Ngonde.(aliyekaa katikati)

Wajumbe wa  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa kikao hicho (kulia wa kwanza )ni Mtendaji wa Mahakama hiyo Bi. Athanasia Kabuyanja, (katikati)  ni Agness  Msani na watatu ni Ferdinad  Kiwonde.i

Wajumbe wa kikao hicho kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Songea wakiendelea kuchambua bajeti yao.

Wajumbe mbalimbali wa kikao hicho  wakiendelea kuchambua bajeti hiyo .          

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni