Na Eunice Lugiana-Mahakama, Kibaha
Katika kuelekea siku ya
wanawake duniani, Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) Wilaya
ya Kibaha, Mkoa wa Pwani, kupitia wawakilishi wake hivi karibuni walitoka elimu
kuhusu masuala mbalimbali ya kifamilia katika wodi ya wazazi kwenye Kituo cha Afya
Mkoani.
Akiongea na wazazi wanasubiria
kujifungua wapatao kumi na mbili (12) kuhusu ukatili, mwakilishi huyo ambaye ni
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Mailimoja, Mhe. Rosely Mwakila alisema vitendo
vya kudharauliwa, kukeketwa pamoja na ubakaji ni ukatili wa kijinsia.
Aliwaomba wazazi hao
endapo wakiona viashiria vya vitendo hivyo watoe taarifa kwenye vyombo husika,
ikiwemo Serikali za Mtaa, Ofisi ya Kata, ustawi wa jamii au Dawati la Jinsia
Polisi.
Wakati huo huo, wito
umetolewa kwa wazazi kuandika majina halisi ya baba wa mtoto pindi wanapojifungua
ili kuepuka usumbufu endapo baba mzazi wa mtoto akifariki.
Wito huo umetolewa na Mwakilishi
wa TAWJA Wilaya ya Kibaha, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Mailimoja, Mhe.
Honorina Kambadu, wakati akiwa katika wodi wa wazazi waliojifungua kwa njia ya
kawaida katika kituo hicho.
Aidha, Mhe. Kambadu
amesema wapo wanawake wanaozaa na wanaume wenye familia na kumficha mtoto ili alisifahamiane
na zake na pia kumpa jina ambalo sio la
baba yake mzazi, hivyo kumnyima haki ya kurithi endapo baba atafariki.
Madaktari na Manesi wa Kituo cha Afya Mkoani wakisikiliza utoaji wa elimu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni