Alhamisi, 30 Machi 2023

‘TUTUMIE RASILIMALI TULIZONAZO KWA UMAKINI’

Na Francisca Swai-Mahakama, Musoma

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Marlin Komba, akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kukagua shughuli za kimahakama wilayani Tarime, amewaasa watumishi wa Mahakama kutumia rasilimali zilizopo kwa umakini ili kuwatumikia wananchi kikamilifu.

Mhe. Komba alitoa rai hiyo baada ya kukagua Mahakama kadhaa katika Wilaya ya Tarime na kujionea namna watumishi wanavyofanya kazi kwa umoja na ushirikiano licha ya uchahe wao, huku shughuli za kimahakama zikiendelea bila kukwama.

Kwa upande wao, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu katika Kanda hiyo, Mhe. Frank Moshi pamoja na Mtendaji wa Mahakama, Bw. Festo Chonya waliunga kauli ya Jaji Komba na kuwataka watumishi kutumia nguvu kazi zilizopo kuhakikisha kazi hazikwami.

Aidha, viongozi hao waliwasisitiza watumishi kufanya kazi kwa moyo, upendo na uadilifu kwani uadilifu unalipa.Waliwahimiza pia kuhakikisha malipo yote yamepokelewa serikalini kabla ya kukatia risiti ya malipo.

Viongozi hao pia walipongeza hatua za utunzaji wa mazingira hasa upandaji miti ambapo katika kipindi hiki cha mvua miti 1,500 imepandwa katika Mahakama za Mwanzo na Mahakama ya Wilaya Tarime.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Marlin Komba (wa tatu kushoto) akikagua mazingira ya Mahakama ya Mwanzo Mtana iliyoko wilayani Tarime.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Marlin Komba akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mahakama katika Kanda ya Musoma, Mahakama Wilaya ya Tarime na watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Mtana.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Marlin Komba (wa tatu kulia) akifafanua jambo baada ya ukaguzi wa Mahakama ya Mwanzo Sirari.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Marlin Komba (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watumishi wa Mahakama, wakiwemo kutoka Mahakama ya Mwanzo Sirari.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Marlin Komba akiwa pamoja na viongozi na watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Nyamwaga wakiangalia na kufurahia mazingira ya Mahakama hiyo.  
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Marlin Komba (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watumishi kutoka Mahakama ya Mwanzo Nyamwaga.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Marlin Komba (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi, wakiwemo watumishi kutoka Mahakama ya Mwanzo Nyamongo.
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Mtana anayetembelea Mahakama ya Mwanzo Nyamwigura, Mhe. Hilda Ang’ulo (aliyesimama) akisoma taarifa ya utendaji kazi wa Mahakama ya Mwanzo Nyamwigura.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Tarime (aliyesimama) akisoma taarifa ya utendaji kazi mbele ya watumishi na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Marlin Komba (hayuko pichani) wakati wa ukaguzi wa Mahakama hiyo.
Naibu Msajili, Mhe. Frank Moshi akisisitiza jambo wakati wa kikao cha watumishi wa Mahakama ya Wilaya Tarime.

 Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Marlin Komba akiwa katika picha ya pamoja ya viongozi na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Tarime.
(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni