Na Magreth Kinabo na
Stanslaus Makendi Mahakama, Dodoma
Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani amesema
kwamba uongozi wa Mahakama ya Tanzania utachukua hatua ya kumwajibisha mtumishi
yoyote yule ambaye atakuwa ni kikwazo wa mabadiliko yanayofanywa na mhimili huo katika kuelekea safari
ya Mahakama Mtandao ifikapo mwaka 2025.
Aidha, Jaji Kiongozi
amewataka Watendaji wa Mahakama mbalimbali kutosita kuwachukulia hatua
watumishi wazembe waliochini yao.
Mhe. Siyani alizungumza
hayo leo tarehe 3 Machi, 2023 wakati
akifunga kikao kazi cha mapitio ya bajeti ya nusu ya
mwaka 2022/23 na uchambuzi wa maandalizi ya bajeti ya mwaka 2023/24 ya Mahakama kilichofanyika Jijini Dodoma,
ambapo alisitiza ushirikiano wa utendaji kazi kwa watumishi hao.
‘‘Hakuna mabadiliko yanaweza kutokea bila uwajibikaji. Kila mmoja wenu
ni lazima atimize wajibu wake kwa vitendo ili kuhakikisha anatimiza jukumu
muhimu la suala la utoaji haki iliyobora kwa usawa na wakati na kuendana na
mabadiliko hayo,’’ alisema Jaji Kiongozi.
Aidha Jaji Siyani aliwataka kushirikiana katika utendaji kazi na kila
mmoja kujiuliza kuwa anaisadiaje Mahakama ya Tanzania katika kusonga mbele na
kupata mafanikio ikiwemo kuondoa fikra kila kitu kitafanywa na Makao Makuu.
‘‘Kila mtu awajibike kwa nafasi yake mnapopanga bajeti vipaumbele viwe
ni vya taasisi.’’ alisisitiza.
Aliwataka Naibu Wasajili na Watendaji wa Mahakama mbalimbali kushirikiana
katika kufanikisha mabadiliko hayo. kwa kuwa mafanikio yatapatikana kutokana na nafasi
ya kila mmoja.
Mhe. Siyani aliongeza kuwa huu ni mwaka wa kufanya mabadiliko ya kutoa
huduma bora, hivyo kila mtu awajibike kwa hilo. Aliongeza kuwa watumishi hao
wanatakiwa kuwa wabunifu ,ikiwemo umiliki wa mabadiliko hayo. Pia wanapaswa
kufahamu utamaduni wa Mahakama.
Kwa upande mwingine, Jaji Kiongozi aliwataka wajumbe wa kikao kazi
hicho, kuangalia vyema namna wanavyopanga bajeti za maeneo yao na kuona ni kwa
jinsi gani wanaweza kuzisaidia Mahakama za Mwanzo kwa kuwa asilimia 70 ya
mashauri yanatoka katika Mahakama hizo.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Viongozi wa Menejimenti ya Mahakama,
Naibu Wasajili, Watendaji wa Mahakama, Mahakimu Wakazi Wafawidhi na Maafisa
Bajeti kutoka Mahakama mbalimbali nchini.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani akitoa hotuba yake leo tarehe 3 Machi, 2023 wakati akifunga kikao kazi cha mapitio ya bajeti ya nusu ya mwaka 2022/23 na uchambuzi wa maandalizi ya bajeti ya mwaka 2023/24 cha Mahakama ya Tanzania kilichofanyika Jijini Dodoma.
Wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja kwenye kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wakiwa katika kikao hicho, wakimsikiliza Jaji Kiongozi.
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert
Chuma akisisitiza jambo kwenye kikao hicho.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Bajeti wa Mahakama mbalimbali nchini. Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson Mdemu (kushoto) na (kulia) ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama mbalimbali nchini. Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson Mdemu (kushoto)na kuliani Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya kikao hicho. Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson Mdemu (kushoto)na kuliani Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Wasajili mbalimbali nchini. Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson Mdemu (kushoto)na kuliani Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma.
(Picha na Mahakama ya Tanzania).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni