Na Aidan Robert-Mahakama, Kigoma
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kigoma, Mhe. Rose Kangwa ameongoza wanawake wa Mahakama katika
Kanda ya Kigoma kusherekea siku ya mwanamke duniani.
Kwa Mkoa wa Kigoma sherehe
hiyo imefanyika katika Kata ya Kidahwe, Wilaya ya Kigoma. Akizungumza katika
hafla hiyo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma, Mhe. Lameck
Mlacha amesema kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake ni nyenzo muhimu kuiwezesha
Kanda hiyo kuwa kinara katika utendaji kazi.
Kauli mbiu ya
maadhimishio hayo inasema Ubunifu na
Mabadiliko ya Teknolojia:Chachu katika kuleta Usawa wa Kijinsia. Alisema siku
hiyo iwe chachu ya maendeleo na kuwainua wanawake kiuchumi na kielimu ili
kujenga uchumi endelevu wa nchi.
Mhe. Mlacha alibainisha
kuwa maendeleo ya teknolojia yakawabadilishe wengi ili watumie muda mwingi
kujijengea uwezo wa kufanya kazi na maendeleo binafsi ya kiuchumi ili kuwa na
maendeleo bora ya familiya na uchumi wa nchi katika kuongeza ubunifu wa mambo
mbalimbali mahali pakazi.
(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Morogoro)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni