Na Evelina Odemba – Mahakama, Morogoro
Wanawake watumishi wa Mahakama ya Tanzania, Kanda ya Morogoro, leo tarehe 8 Machi, 2023 wameungana na wanawake wa mkoani hapa kusherekea siku ya wanawake duniani.
Maadhimiho ya siku hiyo kimkoa yamefanyika katika Wilaya ya Gairo ambayo yamehudhuriwa na watumishi wa Mahakama na viongozi wa kiserikali ngazi ya Mkoa na Wilaya.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, ambaye alitarajiwa kuwa mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mhe. Judith Nguli alitoa rai kwa wanaume kuwaunga mkono wanawake katika jitihada zao za kujiinua kiuchumi, huku akikemea vikali ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
Kauli mbiu ya siku ya wanawake kwa mwaka huu inahusu “ubunifu na mabadiliko ya teknolojia ni chachu katika kuleta usawa wa kijinsia.”
Mahakama ya Tanzania tayari imepiga hatua kwenye upande wa teknolojia ambapo matumizi ya TEHAMA yanashika hatamu kila kukicha ambapo mifumo mipya inabuniwa na kutumika katika shuguli za kimahakama.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mhe. Judith Nguli, akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Jabir Hussein wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama,
Morogoro)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni