-Divisheni ya Ardhi nayo yatoa msaada kwa akina Mama Muhimbili
Na Mary Gwera na Magreth Kinabo
Watumishi wanawake wanaofanya kazi Mahakama ya Tanzania
Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 08 Machi, 2023 wameungana na Wanawake wenzao
wa Mkoa huo kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika
kimkoa katika Viwanja vya Mnazimmoja jijini humo.
Akizungumza na Maelfu ya Wanawake kutoka Ofisi
mbalimbali waliokusanyika katika Viwanja vya Mnazimmoja jijini humo, Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makalla ametoa rai kwa Watanzania kununua kuwaunga
mkono akina Mama wajasiriamali kwa kununua bidhaa zinazozalishwa na wanawake
kwani nyingi zinakidhi ubora hata zaidi ya bidhaa zinazotoka nchi za nje.
“Nachukua
nafasi hii kuwapongeza wanawake kwa siku hii muhimu kwenu, nami kwa kutambua
umuhimu wake nimeona niahirishe shughuli nyingine zote ili nishiriki nanyi, kwa
nafasi hii napenda kuwapongeza pia wajasiriamali wanawake kwa bidhaa nzuri na
hivyo nawaomba wananchi muwaunge mkono kwa kununua bidhaa hizo,” amesema.
Kadhalika, Mhe. Makalla amewataka Wanawake kuendeleza
ushirikiano na mshikamano miongoni mwao ili waweze kupata maendeleo ya dhati na
vilevile kuahidi kuwa Serikali kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kutoa ushirikiano husuani mikopo ili
kuwawezesha wanawake kuendelea na shughuli za uzalishaji mali.
Mkuu huo wa Mkoa ameongeza kuwa, Mkoa wake utaendelea
kuwawezesha kiuchumi wanawake huku akieleza kwamba, Mkoa huo umezindua vikundi
mbalimbali vya VIKOBA ambapo kupitia vikundi hivyo wanawake wameweza kukua
kiuchumi na kufanya maendeleo kadha wa kadha.
“Naomba mpuuze maneno yanayosemwa na baadhi ya Wanasiasa
kuhusu VIKOBA, mtu anayezungumzia vibaya kuhusu VIKOBA hajui umaskini ulivyo na
maana, hivyo endeleeni na tutaendelea kuvizindua vingi zaidi,” amesisitiza Mhe.
Makalla.
Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
kwa mwaka huu, 2023 inasema; ‘Ubunifu na mabadiliko ya Teknolojia ni chachu
katika kuleta usawa wa kijinsia,’.
Wakati
huohuo, Watumishi
wanawake wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Ardhi wakiongozwa na Jaji
Mfawidhi wa Mahakama hiyo Mhe. Agnes Mgeyekwa katika kusherekea siku hiyo wameungana wanawake waliolazwa
na watoto wao kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kutoa msaada wa vitu
mbalimbali.
Wanawake
wa Mahakama hiyo wametoa msaada
wa vitu mbalimbali kwa wakinamama hao, ambavyo ni pamoja na sabuni za kuogea na kufulia, mafuta ya kujipaka, miswaki, dawa ya
meno, taulo za kike na nepi za Watoto (diapers).
Akizungumzia
kuhusu siku hiyo, Jaji wa Mahakama ya Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Ardhi, Mhe.
Arafa Msafiri amesema
wanawake wa Mahakama hiyo wametoa msaada wa vitu hivyo, ikiwa ni ishara ya
kuonesha upendo kwao.
Vitu
hivyo vilikabidhiwa kwa wanawake hao, kupitia
Usimamizi wa Parokia ya Muhimbili Somo Bikira Maria Salama ya Wagonjwa) chini
ya Padri
Athanas Bwakila, ambaye alishukuru kwa msaada huo, huku akisema bado wakinamama wana
mahitaji yao ni makubwa na wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo madeni
ya matibabu, ambapo aliwaomba watu wengine kuiga mfano huo wa kuwasaidia
wahitaji hao.
Padre
Bwakila aliwashauri wanawake wote kuwa waadhimishe siku hiyo kwa kukumbushana
kulea familia zao vizuri ili ziweze kuwa na maadili mema.
Kwa
upande wa Mahakama Kuu Masjala Kuu, Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es
Salaam na Mahakama Kuu Kituo cha cha Usuluhishi wameadhimisha siku hiyo kwa
kukumbushana mambo mbalimbali, mgeni rasmi alikuwa ni Jaji wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, Divisheni ya Ardhi, Mhe. Dkt.Benhajj Masoud.
Akizungumzia
kuhusu siku hiyo, Jaji Masoud alisema ni muhimu kukumbuka na kuzingatia kuwa
kila siku ni siku ya wanawake kwa muktadha wa nafasi ya wanawake na mchango wa
wanawake katika maendeleo na kila kitu kwenye maisha ya kila mmoja.
‘‘Hata
hivyo, tunapoadhimisha siku hii adhimu na muhimu hatuna budi kukumbuka uwepo wa vitendo vya
kinyanyasaji na kibaguzi wanavyofanyiwa wanawake kila siku na hivyo uwepo wa
haja na kuzidisha kuongeza jitihada na maarifa kwenye vita ya kukabiliana na
tatizo hili, zikiwemo changamoto zake,’’amesisitiza huku akisema vita hiyo iwe
endelevu.
Jaji
Masoud ameongeza
kwamba ubunifu na matumizi sahihi ya mabadiliko ya teknolojia yanaifanya
teknolojia iondoe vikwazo ambavyo wanawake wengi walikuwa wakikabiliana navyo
katika nyanja zote za misha, kijamii, kiuchumi na kisiasa.Pia teknolojia
inasaidia kuhabarisha umma kuhusu vitendo vinavyoathiri usawa wa kijinsia na
nmna bora ya kukabiliana navyo.
Amesema teknolojia inaleta wepesi wa
kufikia na kupata haki na hivyo urahisi wa kukabiliana na vitendo vya
unyanyasaji wa kijinsia, inaleta wepesi na fursa za kiujasiriamali na ajira.
Wanawake hao pia walikumbushana kuwa na umiliki wa mali, ubunifu, kujiamini, kushirikiana na kujenga uthubutu wa kufanya mambo mbalimbali.
MATUKIO KATIKA PICHA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE
DUNIANI MKOA WA DAR ES SALAAM
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makalla ambaye
alikuwa Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mkoa wa
Dar es Salaam akitoa hotuba yake wakati wa Sherehe hizo zilizofanyika leo
katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Katika picha ni sehemu ya Watumishi Wanawake wanaofanya kazi Mahakama ya Rufani wakiwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam zilipofanyika Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo tarehe 08 Machi, 2023.
Sehemu ya Watumishi wanawake wa Mahakama ya Rufani (T)
wakiwa katika picha ya pamoja katika Viwanja vya Mnazi Mmoja zilipofanyikia
sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kimkoa.
Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu (ADHR)-Mahakama
ya Tanzania, Bi. Agnes Kavishe (katikati) akikata keki maalum iliyoandaliwa kwa
Watumishi Wanawake wa Mahakama ya Rufani ikiwa ni ishara ya kusherehekea Maadhimisho
ya Siku ya Wanawake Duniani. Wanaoshuhudia ni Maafisa Utumishi wa Mahakama.
Sehemu ya Watumishi wa Mahakama ya Rufani Wanawake
wakiwa kwenye hafla fupi ya kusherehekea Siku ya Wanawake Dunia iliyofanyika
katika Ukumbi wa Maktaba uliopo katika Mahakama hiyo.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Ardhi, Mhe. Arafa Msafiri (aliyenyoosha mikono) akizungumza na baadhi ya wakina mama waliolazwa na watoto wao katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo wakati Watumishi wanawake wa Divisheni hiyo walipofika hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali. Katikati ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, Mhe. Agness Mgeyekwa na kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, Mhe. Dkt. Theodora Mwenegoha.
Baadhi ya vitu mbalimbali vilivyotolewa msaada na Mahakama hiyo kwa wakina mama waliolazwa na watoto wao katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Padri Atanas Bwakila (mwenye joho jeupe) akizungumza na baadhi ya wanawake Mahakama hiyo.
Baadhi ya wanawake wa Mahakama hiyo wakimsikiliza Padri.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Ardhi, Mhe. Agatha Chugulu akitoa neno la Shukrani.
Mkuu wa Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Tumaini (TUDARCo), Bi. Lois-Singa Metili akitoa Mada ya Ujasiriamali na Ubunifu kwa Watumishi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi wakati ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani leo tarehe 08 Machi, 2023.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, Mhe. Agness Mgeyekwa (katikati) pamoja na sehemu ya Watumishi wa Divisheni hiyo wakikata keki kusherehekea Sikukuu ya Siku ya Wanawake Duniani.
Baadhi ya wanawake wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu, Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam na
Mahakama Kuu Kituo cha Usuluhishi wakifurahia leo Siku ya Wanawake Duniani katika hafla fupi iliyofanyika
katika ukumbi wa Mahakama Kuu ya Tanzania-Dar es Salaam.
Kaimu Jaji Kiongozi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sekela Moshi, akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Kaimu Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sekela Moshi (kulia), akimlisha keki mgeni rasmi Mhe. Dkt. Benhaji Masoud wakati wa hafla fupi ya kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni