Na Evelina Odemba – Mahakama Morogoro.
Timu ya michezo ya Mahakama ya Tanzania (Mahakama Sports) jana tarehe 15 Aprili, 2023 iliwasili mkoani Morogoro tayari kushiriki michezo ya Mei Mosi.
Michezo hiyo ambayo kitaifa itafanyikia mkoani hapa katika uwanja wa Jamuhuri ulioko Mkoani Morogoro huku timu ya Mahakama ikiwa imejinoa kunyakua vikombe vipya katika michuano hiyo ikiwa ni sanjari na kutetea ubingwa walioupata mwaka 2022 katika Mashindano hayo ya Mei Mosi.
Akizungumza baada ya kuwasiri, Katibu Mkuu wa Mahakama Sports Robert Tende alisema kuwa Mahakama Sports imejipanga vizuri kushikiri michuano hiyo na wachezaji wote tayari wapo kambini wanasubiri filimbi ilie ili waingie uwanjani kuipatia Mahakama ya Tanzania ushindi mkubwa.
Akituma salamu kwa
timu watakazokutana nazo uwanjani, Tende alisema kuwa “tumefanya maadalizi ya
kutosha, tuna wachezaji wazuri wenye
morali wanasubiri muda tu kuonesha maajabu na awamu hii tutashiriki
michezo mingi zaidi tofauti na ilivyokuwa Mei Mosi iliyopita” alieleza.
Aliitaja michezo watakayoshiriki kwa msimu huu ni Kamba wanaume na Kamba wanawake, Mpira wa Miguu wanaume, Mpira wa Pete wanawake, mashindano ya riadha, bao, karata na mchezo wa drafti.
Aidha, Tende alitoa shukurani zake za dhati kwa uongozi wa Mahakama kwa kuwawezesha kushiriki kwa wingi na kushiriki michezo mbalimbali sanjari na mara nyingi wamekuwa wakishiriki kuwafunda wachezaji na hali hiyo imepelekea timu za Mahakama kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.
“Nitoe shukrani zangu za dhati kwa uongozi mzima wa Mahakama ya Tanzania kwa kuanza na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahimu Juma, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel na Mkurugenzi wa Rasmali watu wa Mahakama ya Tanzania Beatrice Patrick kwa mchango wao mkubwa kutufanikisha kushiriki kwa wingi katika michezo hii na kuitangaza Mahakama ya Tanzania upande wa michezo” aliongeza Tende.
Tende alihitimisha kwa kutoa rai yake kwa wana Mahakama Sports wawe na nidhamu na kujituma zaidi kwakuwa wanaiwakilisha Mahakama ya Tanzania katika michezo, hivyo waitumie fulsa hiyo kama sehemu ya kuitangaza Mahakama ya Tanzania.
Michezo ya Mei Mosi
kuhitimishwa tarehe 29 Aprili, 2023 imekuwa ikishirikisha wanamichezo ambao ni
watumishi kutoka idara za serikari, Wizara, Mashirika ya Umma na Binafsi,
taasisi za Serikali na Binafsi bila kusahau Majeshi ya Tanzania ambayo imekuwa
ikiwaleta pamoja watumishi na kwa mwaka 2023 kauli mbiu ni “Mishahara Bora na
Ajira za Staha ni Nguzo kwa Maendeleo ya wafanyakazi, wakati ni sasa.”
Katibu Mkuu wa Klabu ya Timu ya Mahakama Bwana Robert
Tende akifafanu jambo mara baada ya kufika kwenye kambi kwa ajili ya kushiriki
michezo ya Mei Mosi.
Baadhi ya washiriki kutoka Mahakama Sports Club wakiwa
katika picha ya pamoja mara baaada ya kuwasili kambini.
Viongozi wa Mahakama Sports wakiwa wanaweka mikakati sawa mara baada ya kuwasili ilipo kambi ya wananamichezo toka Mahakama.
Sehemu ya vifaa vya wanamichezo vikiwa tayari kugawiwa kwa wanamichezo hao.
“Tunapumzika kidogo” baadhi ya wanamichezo toka timu ya Mahakama Sports wakivuta pumzi mara baada ya kuwasili ili kushiriki michuano ya mei mosi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni