Na Mwandishi wetu-Mahakama, Dar es Salaam
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam hivi
karibuni iliendesha mafunzo ya mfumo wa kuratibu mashauri ulioboreshwa (e-CMS).
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Kinondoni. Wakufunzi wa mafunzo hayo walikuwa
Afisa Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
salaam, Elisia Meela, Afisa TEHAMA IJC Kinondoni Delphina Mwakyusa.
Maafisa hao walisaidiwa na Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe.Sundi Fimbo na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kivukoni, Mhe. Franco Kiswaga.
Mafunzo hayo yalifunguliwa kwa njia ya mkutano mtandao
‘video conference’ na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam, Mhe.Salma
Maghimbi, ambaye alikuwa jijini Mwanza.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es salaam, Mhe.Salma Maghimbi, akifungua mafunzo kwa njia ya mkutano mtandao akiwa jijini Mwanza kuhusu mfumo wa kuratibu mashauri ulioboreshwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni