Na Francisca Swai – Mahakama, Musoma
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma Mhe. Frank Moshi amewataka watumishi na wadau wa Mahakama katika kanda hiyo kuwa na matumizi sahihi ya mifumo ya kielektroniki katika usikilizaji wa mashauri ili kuwawezesha wananchi kupata huduma za utoaji haki popote walipo.
Mhe.Moshi alizungumza hayo hivi karibuni alipokuwa akifundisha juu ya matumizi ya mfumo mpya ulioboreshwa wa Usimamizi wa Mashauri Kilektroniki (e- Case Management System), ambapo alisema mifumo iliyopo mahakamani ni hatua ya kutekeleza Mpango Mkakati wa Mahakama wa mwaka 2021/22 – 2024/25 unaomlenga mwananchi na kushirikisha wadau katika kuhakikisha haki inatolewa kwa wakati.
“Mahakama imejikita katika mtumizi ya mifumo mbalimbali ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuhakikisha mwananchi popote alipo anafikiwa na kupata kile anachohitaji kwa wakati na kwa usahihi. Hivyo mafunzo haya ya mfumo huu mpya ulioboreshwa wa Usimamizi wa Mashauri Kielektroniki (e- Case Management System) uwe chachu ya kuujulisha umma mahali Mahakama ilipofikia na ndio maana wadau wameshirikishwa moja kwa moja ili wote twende sambamba,” alisema Moshi.
Katika mafunzo hayo watumishi na wadau wa Mahakama walielekezwa namna ya kutumia mfumo huo mpya ambapo waliweza kujionea faida zake ikiwemo namna utakavyo rahisisha utoaji wa haki kwa kupunguza gharama na muda kwenye usikilizwaji wa shauri tangu linapofunguliwa hadi kuamuliwa, ikiwemo kutapunguza mlolongo wa watu kwani tangu shauri linafunguliwa hadi kukamilika hatua zote zitafanyika kielektroniki.
Alitaja faida nyingine ni kupunguza matumizi ya karatasi ambazo zinaweza kupotea au kuharibika kwa urahisi, hivyo kuufanya mfumo kuwa wakuaminika zaidi, utamsaidia mteja kupata mwenendo wa shauri lake pamoja na hukumu ndani ya wakati, pia mteja ataweza kupata nakala yake ya hukumu katika lugha anayoipendelea yeye ya Kishwahili au Kingereza.
Mafunzo hayo yaliongozwa na Moshi kwa kushirikiana na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma Mhe. Erick Marley pamoja na Afisa TEHAMA wa Kanda hiyo Bw. Simon Lyova yalifanyika Wilayani Tarime tarehe 12 Aprili, 2023, yaliihusisha watumishi na wadau kutoka Wilaya za Tarime, Serengeti na Rorya. Pia yalihitimishwa Mahakama Kuu Musoma tarehe 14 – 15 Aprili 2023, ambapo yalihusisha wadau na watumishi wa Mahakama wa Wilaya za Musoma, Bunda na Butiama.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma, Mhe Frank Moshi (aliyesimama) akielezea jambo kwa washiriki wakati wa mafunzo ya matumizi ya mfumo mpya ulioboreshwa wa Usimamizi wa Mashauri kielektroniki (e- Case Management System) yaliyofanyika Mahakama Kuu Musoma.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma Mhe, Erick Marley (aliyesimama) akielezea jambo kwa washiriki wakati wa mafunzo ya matumizi ya mfumo mpya ulioboreshwa wa Usimamizi wa Mashauri kielektroniki (e- Case Management System) yaliyofanyika Mahakama Kuu Musoma.
Wakili Ostach Mligo na Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili wa Kujitegemea (TLS) chapta ya Musoma (aliyekaa katikati)pamoja na wadau wengine wakifurahia mafunzo kwa vitendo juu ya matumizi ya mfumo mpya ulioboreshwa wa Usimamizi wa Mashauri kielektroniki (e- Case Management System) yaliyofanyika Mahakama Kuu Musoma
Mawakili wa Serikali pamoja na Mawakili wa kujitegemea wakifanya mafunzo kwa vitendo juu ya matumizi ya Mfumo mpya ulioboreshwa wa Usimamizi wa Mashauri kielektroniki (e- Case Management System) yaliyofanyika Mahakama Kuu Musoma.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Bunda Mhe. Mulokozi Kamuntu (aliyekaa wa pili kulia), Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Butiama Mhe. Judith Semkiwa(aliyekaa wa kwanza kulia) pamoja na watumishi wengine wa Mahakama wakiendelea na mafunzo kwa vitendo juu ya matumizi ya mfumo mpya ulioboreshwa wa Usimamizi wa Mashauri kielektroniki (e- Case Management System) yaliyofanyika Mahakama Kuu Musoma
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Musoma Mhe. Aristida Tarimo (aliyekaa wa kwanza kushoto mwenye Tsheti ya rangi ya bluu), Hakimu Mkazi Mahakama ya Musoma Mhe. Hadija Masala (aliyekaa wa kwanza kulia) pamoja na watumishi wengine wa Mahakama wakiendelea na mafunzo kwa vitendo juu ya matumizi ya mfumo mpya ulioboreshwa wa Usimamizi wa Mashauri kielektroniki (e- Case Management System) yaliyofanyika Mahakama Kuu Musoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni