Na Evelina Odemba – Mahakama Morogoro
Timu za kuvuta Kamba toka Klabu ya Mahakama Sports leo tarehe 19 Aprili 2023 imeibuka kidedea dhidi ya wapinzani wao ni katika hatua ya makundi kwenye michuano ya kuwania Kombe la Mei Mosi inayoendelea mkoani Morogoro.
Timu hizo zilizoshuka dimbani katika uwanja wa Jamhuri ambapo upande wa wanaume walivutana na timu kutoka kilimo wakati upande wa wanawake walivutana na timu kutoka Madini na makundi haya yote ya timu (Me) na (Ke) upande wa Mahakama yaliibuka washindi baada ya kuwavuta wapinzani wao dakika chache tu baada ya kipenga kulia hali iliyoonesha kuwa Mahakama awamu hii wamejiandaa kuutwaa ubingwa wa nafasi ya kwanza.
Mashindano hayo yaliyoibua hisia za watazamaji kuona jinsi ambavyo Mahakama imejipanga na hata wapinzani wao upande wa timu ya kilimo ambao waliomba nafasi ya kupiga picha ya pamoja na Timu ya Mahakama huku wakijipongeza kushindana na Mahakama wakati huo huo Kepteni wa timu ya kilimo ambaye jina lake halikupatikana alisikika akisema kuwa, “Timu ya Kamba toka Mahakama ipo vizuri hata hatujisikii vibaya kuupoteza mchezo huu kwani tumepangwa na timu kubwa” alisema.
Kwa upande wa mpira ya pete timu ya mahakama ilipoteza mchezo wake dhidi ya timu ya mawasiliano ambayo ilishinda kwa magoli 20 kwa 18 waliyopata Mahakama, hata hivyo licha ya kutofua dafu katika mchezo huo bado kocha Adam Adam amesisitiza kuwa mahakama inafanya vizuri katika mchezo wa pete na kadili mashindano yanavyoendelea imezidi kuonesha viwango bora vya uchezaji tofauti na ilivyokuwa mara ya kwanza.
Sambamba na kuibuka washindi katika mashindano ya leo bado Mahakama Sports Klabu imeingia uwanjani kwenye mazoezi ya kujiandaa kwa ajili ya siku ya kesho tarehe 20 Aprili, 2023 ambapo timu zake mbalimbali zitashuka katika viwanja vya michezo tofauti tofauti katika hatua za makundi.
Timu zitakazoshuka viwanjani ni timu ya mpira wa miguu itakayocheza na timu ya mawasiliano katika uwanja wa Jamhuri, timu ya mpira wa pete itakayoshuka dimbani na timu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika viwanja vya Bwalo wakati timu ya kamba upande wa wanaume inajifua kushuka dimbani na timu toka Ikulu.
Timu ya kuvuta Kamba Wanaume toka Mahakama itakayoshiriki michezo ya kuwania kombe la mei mosi.
(Picha na Evelina Odemba).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni